Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, marhum al-Jundi ambaye pia alikuwa kiongozi katika Jumuiya ya Wasomaji Qur'ani katika mkoa wa Beni Suef ulio kati mwa Misri alifikia mwisho mwema katika umri wake pale alipoadhini na baada ya hapo kuaga dunia.
Taarifa zinasema marhum aliadhini katika Msikiti wa Abu al-Saud katika eneo la Nasr kaskazini mwa Beni Suef na baada ya kuadhini aliketi na kuegemea katika ukuta msikitni hapo na baada ya dakika kadhaa ulipofuka muda wa Sala hadhirina walimtaka aswalishe lakini hakujibu na hivyo alikimbizwa hospitaliani. Alipofika hospitalini, madakatari walisema kuwa ameshaaga dunia.
Marhum al Jundi alikuwa kati ya wasomaji bora zaidi wa Qur'ani katika mkoa wa Beni Suef na alikuwa kipenzi cha watu wa mkoa huo. Tunamuomba Allah ampe safari ya wepesi kaburi lake liwe miongoni mwa bustani za Peponi na Allah amjaalie Makaazi mema katika Pepo.
3673293