IQNA

Al Azhar kutumia mbinu ya kielektroniki kufunza kuhifadhi Qur'ani Tukufu

19:09 - September 30, 2019
Habari ID: 3472154
TEHRAN (IQNA)- Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri kimetangaza mpango wa kuwawezesha vijana kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa kutumia programu ya kompyuta inayojulikana kama 'Kitabu cha Kielektroniki'.

Kwa mujibu wa taarifa Al Azhar inatumia sauti ya qarii maarufu wa Qur'ani duniani marehemu Shaykh Mahmoud Khalil al-Husary, baada ya kupata idhini ya familia yake,  katika programu hiyo ya kompyuta. Mradi huo ulianza mwaka moja uliopita.

Fayez Nasr, mkuu wa masomo kwa njia ya kompyuta katika Chuo Kikuu cha Al Azhar amesema programu hiyo itatekeleza na Idara ya Elimu ya Kompyuta chuoni hapo.

Aidha amesema mradi huo unatekelezwa katika awamu tatu ambapo awamu ya kwanza inawalenga wanafunzi wa shule za msingi. Programu hiyo ya shule za msingi pia ina tafsiri sahali kwa wanafunzi. Awamu ya pili ni ya wanafunzi za shule za upili na pia imewekwa katika tovuti ya Al Azhar ili mtu yeyote anayetaka aweze kuitumia.

Msomi wa Al Azhar, Sheikh Amed Tag El Din anasema 'Kitabu cha Kielektroniki' ni katika jitihada za hivi karibuni kabisa za Al Azhar kuwasaidia wanafunzi kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa kutumia teknolojia ya kisasa. Amesema moja kati ya nukta chanya za programu hiyo ni usahali wake kwa wanafunzi.

3845969

captcha