IQNA

Trump alitaka kuwatimua Waislamu, sasa wakati wa COVID-19 Waislamu wananusuru maisha

16:06 - December 29, 2020
Habari ID: 3473503
TEHRAN (IQNA) – Januari 27 2017 ni siku ambayo Waislamu Wamarekani hawataishau. Katika siku hiyo, Rais Donald Trump wa Marekani alitia saini dikrii ya kuwapiga marufuku Waislamu nchini humo.

Hii ilikuwa hatua ya kwanza ya kibaguzi ya Trump dhidi ya wahajiri wa kigeni nchini humo ambapo alizitenganisha maelfu ya familia. Watu wengi ambao walikuwa na kadi ya kijani maarufu kama Green Card, ambayo iliwapa haki ya kuishi Marekani, walikamatwa na kurejeshwa nchi zao za asili. Trump alikuwa amekusudia kuwatimua Waislamu nchini humo.

Sasa, zaidi ya miaka miwili baada ya Trump kuwatimua Waislamu na kuwazuia Waislamu kutoka nchi zaidi ya sita kuingia nchini humo, Marekani, sawa na maeneo mengine duniani, imekumbwa na janga la COVID-19 au corona. Hadi sasa zaidi ya watu milioni 19 wameambukizwa corona Marekani na wengine 333,000 wamefariki. Duniani kote pia karibu watu milioni 1.7 wamefariki na zaidi ya milioni 80 wameambukizwa ugonjwa huo.

Lakini sasa kuna matumaini ambayo yamejitokeza baada ya kupatikana chanjo ya corona. Wavumbuzi wa chanjo ya corona ambayo inategemewa sana Marekani na duniani kote  ni wanandoa Waislamu wenye asili ya Uturuki ambao wanaishi Ujerumani.  Bw. Ugur Sahin, Mturuki ambaye alihamia Ujerumani na Bi. Ozlem Tureci, bintiye daktari Mturuki aliyeahmia Ujerumani kutoka Istanbul Uturuki, ndio ambao wamegundia chanjo ya corona inayotumika Marekani.

Daktari Sahin alitunukiwa ya Zawadi ya Mustafa SAW mwaka 2019. Hii ni zawadi  ambayo Iran huwatunuku wanasayansi bora zaidi Waislamu duniani kila miaka miwili.

Wanasayansi hao wawili Waislamu walianzisha shirika la BioNTech ambalo limeshirikiana na Shirika la Pfizer kutengeneza chanjo ya COVID-19 ambayo imefanikiwa kwa kiwango cha zaidi ya asilimia 90 na sasa imesambazwa kwa wingi Marekani kwa lengo la kuangamiza kirusi cha corona. Chanjo hiyo iliyotegenezwa na wanasayansi hao Waislamu inatumiwa pamoja na nyingine inayojulikana kama Moderna. Mwanasayansi mwengine Mwsilamu aliye mstari wa mbele katika vita dhidi ya COVID-19 nchini Marekani ni Daktari Moncef Slaoui ambaye asili yake ni Morcco. Yeye ni mshauri mkuu katika mradi wa serikali ya Marekani wa Operation Warp Speed ambao unaleta pamoja sekta binafsi na sekta ya umma katika kuharakisha utafiti, ustawi, utegenezwaji na usambazwaji wa chanjo za COVID-19.

Chanjo hiyo ya BioNTech-Pfizer pia ndiyo inayotegemewa kwa wingi barani Ulaya pamoja na kuwa bara hilo nalo limekuwa kitovu cha chuki dhidi ya Waislamu na Uislamu.

Mwanaharakati wa Kiislamu Marekani Lallia Allali anasema vyombo vya habari Marekani havitaki kutaja kuwa Waislamu wako mstari wa mbele kukabiliana na COVID-19 na hivyo kuokoa maisha ya mamilioni lakini wakat kunapojiri tukio la kigaidi, vyombo hivyo vya habari hufanya juu chini kunasibisha tukio kama hilo na Uislamu au Waislamu.

3473545

captcha