IQNA

Ayatullah Ramadhani

Imam Khomeini alihuisha fikra ya Kiislamu ya kupinga ubeberu

12:10 - February 04, 2021
Habari ID: 3473620
TEHRAN (IQNA) – Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (AS) amesema Imam Khomeini, Mwenyezi Mungu Amrehemu, alihuisha fikra ya Kiislamu ya kupinga ubeberu au ukoloni wakati ambao madola mengi ya kibeberu yalikuwa yanajaribu kusambaratisha kabisa fikra hiyo.

Akizungumza katika warsha ya kimataifa iliyofanyika kwa njia ya intaneti (webinar), wakati huu wa maadhimisho ya mwaka wa 42 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ridha Ramadhani, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (AS) ameongeza kuwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yameonyesha kuwa dini inaweza kuwa na mfumo uliofanikiwa wa kisiasa hata katika zama hizi za kisasa.

Ameongeza kuwa aghalabu ya mapinduzi duniani na ya kisekula au hayana msingi wowote wa kidni lakini Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yaliwasilisha fiqhi mpya ya kisiasa.

Ameongeza kuwa baadhi ya watu walikuwa na dhana potovu kuwa dini haina nafasi katika zama hizi za sayansi na teknolojia lakini "Imam Khomeini MA alifanya kazi kubwa ya kuoneysha kuwa hakuna chochote kinachoweza kuchukua nafasi ya dini katika uga wa kisiasa na kijamii na kwa msingi huo, harakati ya Imam inaweza kutajwa kuwa muujiza wa karne."

3951782

captcha