IQNA

Khatibu wa Msikiti wa Al Aqsa ataka Waislamu waungane kuhusu mwezi mwandamo wa Ramadhani

18:20 - April 09, 2021
Habari ID: 3473795
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) amesisitiza kuhusu udharura wa kuungana Waislamu katika kutangaza mwezi mwandamo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Katika hotuba yake ya Sala ya Ijumaa leo, Sheikh Mohammad Salim amependekeza kuwa taasisi za kutoa fatwa katika nchi za Kiislamu ziwe na umoja katika kadhia hii ili umoja wa Waislamu uweze kudhihirika.

Leo maelfu ya Waislamu Wapalestina wamemiminika katika Msikiti wa Al Aqsa kwa ajili ya Sala ya Ijumaa ya Mwisho kabla ya kuwadia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel, ambao unakaliwa kwa mabavu mji wa Quds, wamezuia idadi kubwa ya Waislamu kushiriki katika sala hiyo.

Pamoja na hayo, Idara ya Wakfu wa Kiislamu katika Quds Tukufu imesema takribani Waislamu 40,000 wameweza kushiriki katika Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al Aqsa.

Sheikh Mohammad Salim ametoa wito kwa nchi za Kiislamu na Kiarabu ziwaunga mkono Wapalestina kwa kukata uhusiano wowote ule na adui Mzayuni.

3963305

captcha