IQNA

Msikiti walengwa katika tukio la chuki dhidi ya Uislamu nchini Ufaransa

21:28 - April 12, 2021
Habari ID: 3473805
TEHRAN (IQNA)- Katika mfululizo wa hujuma na mashambulizi yanayolenga matukufu ya Waislamu na maeneo yao ya ibada nchini Ufaransa, watu wasiojulikana wameuvunjia heshima msikiti wa Waislamu katika mji wa Reims.

Msikiti walengwa katika tukio la chuki dhidi ya Uislamu nchini UfaransaKwa mujibu wa taarifa, siku mbili tu kabla ya kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani, mtu au watu wasiojulikana wamechora nembo na maneno yanayovunjia heshima matukufu ya Kiislamu na kueneza propaganda chafu dhidi ya dini hiyo katika kuta za Msikiti wa mji wa Reims.
Hujuma hiyo imelaaniwa na Waziri wa Mambo ya Ndani na vilevile Meya wa mji wa Reims ulioko Kaskazini Mashariki mwa Ufaransa.
Hujuma na mashambulizi kama haya yanachochewa na misimamo na maamuzi yanayochukuliwa na serikali na viongozi wa Ufaransa dhidi ya Waislamu. Hivi karibuni Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa alitoa matamshi yanayokinzana na kaida za kidiplomasia na kidemokrasia na kutangaza kuwa, Ufaransa itaendelea kuonyesha katuni na vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW.
Matamshi hayo ya Rais wa Ufaransa yamekosolewa sana na Waislamu, wasomi na wanasiasa katika maeneo mbalimbali ya dunia.
Hivi karibuni pia Baraza la Seneti la Ufaransa lilipasisha marufuku ya vazi la Hijabu kwa wasichana wa Kiislamu wenye umri wa chini ya miaka 18. Baraza hilo pia limezidisha kifungu kingine katika azimio hilo ambacho kinapiga marufuku kutekeleza ibada na desturi za kidini katika vyuo vikuu vya Ufaransa. Muswada wa zimio hilo ulipendekezwa mwaka jana na Rais Emmanuel Macron na limekosolewa sana ndani ya nje ya nchi hiyo kutokana na kuwabana na kuwakandamiza Waislamu.

3474432

captcha