IQNA

Msikiti wa Tokyo waandaliwa kwa ajili ya Ramadhani

22:17 - April 13, 2021
Habari ID: 3473810
TEHRAN (IQNA)- Msikiti wa Tokyo, Japan umeandaliwa kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani huku hatua zikichukuliwa kuzuia kuenea COVID-19.

Kwa mujibu wa Muhammed Rasid Alas, mshauri wa masuala ya kijamii katika Ubalozi wa Uturuki, Msikiti wa Tokyo umeandaa vikao vya kusoma Qur’ani Tukufu na mafunzo ya kuswali kwa watoto kwa njia ya intaneti.

Amesema washiriki watakuwa kutoka jamii Waislamu kutoka mataifa mbali mbali ambao wanaishi katika mji mkuu huo wa Japan. Kwa msingi huo mijimuiko hiyo kwa njia ya intaneti itafanyika kwa njia mbali mbali.

Kutokana na janga la COVID-19 hakutakuwa na mijumuiko ya futari msikitini Japan katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Hatahivyo kutakuwa na Sala ya Tarawih misikitni kwa kuzingatia kaununi za COVID-19 kama vile kutokaribiana, kuvaa barakoa na kila mtu kuja na mkeka wake wa kuswali.

3474445

captcha