IQNA

Utawala wa Kizayuni waanzisha mashambulizi ya angani, nchi kavu dhidi ya Ghaza

12:34 - April 16, 2021
Habari ID: 3473819
TEHRAN (IQNA)- Jeshi la utawala haramu wa Israel zimetekeleza mashambulizi ya angani na nchi kavu dhidi ya eneo la Ukanda wa Ghaza mapema leo asubuhi.

Kwa mujibu wa duru za Palestina, ndege hizo za kivita za Israel zimedondosha mabomu katika eneo la kaskazini mwa Ukadna wa Ghaza. Aidha taarifa zaidi zinasema jeshi la Israel limevurumisha makombora katika eneo la Hjar al Dik katika Ukanda wa Ghaza.

Utawala wa Kizayuni wa Israel umedai kuwa mashambulizi hayo ni jibu kwa maroketi yaliyovurumishwa kutoka Ghaza na kulenga ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

Ndege za kivita, helikopta, droni na vifaru  vya utawala wa Kizayuni katika miezi ya karibuni zimefanya hujuma kwa mara kadhaa katika Ukanda wa Ghaza. 

Malefu ya Wapalestina wasio na hatia wameuawa na kujeruhiwa katika mashambulizi ya Israel dhidi ya Ghaza.

Eneo la Ukanda wa Ghaza liko chini ya mzingiro wa anga, nchi kavu na baharini wa Israel tangu mwaka 2006 na hivyo kuwasababishia matatizo na masaibu mengi wakazi wa Kipalestina wa eneo hilo. 

Wapalestina wanasisitiza kuwa hawatasalimu amri mbele ya matakwa ya utawala wa Kizayuni wa Israel na wana azma imara ya kuendeleza mapambano hadi watakapokomboa ardhi zao.

3474465

captcha