IQNA

Magaidi waua Waislamu 19 msikitini nchini Niger

18:27 - April 19, 2021
Habari ID: 3473831
TEHRAN (IQNA)- Magaidi wameua Waislamu 19 waliokuwa msikitini nchini Nigeria katika eneo la mpaka wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika na Mali.

Kwa mujibu wa taarifa, magaidi hao wakufurishaji walihujumu waumuni hao katika kijiji cha Gaigorou katika jimbo la Tillaberi. Eneo hilo limekuwa likishambuliwa na magaidi wakufurishaji mara kwa mara tokea mwezi Januari mwaka huu.

Gavana wa jimbo hilo Ibrahim Tidjani Katiella amenukuliwa akisema yumkini waliotekeleza shambulio hilo waliingia kinyemela nchini humo wakitokea Mali.

Waziri wa Ulinzi wa Niger Alkassoum Indatou amewaambia wakazi wa eneo hilo kuwa serikali itaendelea kupambana na magaidi nguvu.

Afisa mmoja wa Manispaa ya Dessa ameliambia shirika la habari la AFP kuwa, wavamizi hao huku wakiwa wamefuka nyuso zao na wakiwa juu pikipiki walishambulia kijiji cha Gaigarou usiku wa kuamkia jana na kuanza kufyatua risasi ovyo.

Amesema wavamizi hao waliushambulia mkusanyiko wa wanakijiji waliokuwa wamejumuika kwa ajili ya mazishi, na kisha wakaaza kumpiga risasi kila aliyekuwa mbele yao. Watu kadhaa wamejeruhiwa pia katika shambulio hilo.Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na hujuma hiyo.

Niger imekuwa ikishambuliwa na magaidi wakufurishaji wanaofungamna na kundi la ISIS. Hujuma hizo za kigaidi ni tishio kwa rais mpya wa Niger Mohamed Bazoum ambaye aliapishwa mapema mwezi huu siku chache tu baada ya baadhi ya wanajeshi kufanya jaribio la mapinduzi katika ikulu iliyoko mji mkuu, Niamey.

/3474494

Kishikizo: niger magaidi isis
captcha