IQNA

Ramadhani ni mwezi wa kujiboresha na kuboresha jamii + Video

21:27 - April 20, 2021
Habari ID: 3473832
TEHRAN (IQNA)-Mwezi Mtukufu wa Ramadhani si tu kuwa ni fursa ya Muislamu kujijenga na kujiboresha bali pia ni fursa ya kuiboresha jamii.

Hayo yamesemwa na Hujjatul Islam Muhsin Radmard mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW nchini Marekani na Canada.

Katika Uislamu na hasa katika madhehebu ya Shia, Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unapewa hadhi ya juu sana na ya kipekee. “Si tu kuwa huu ni mwezi wa Muislamu kujiboresha bali pia ni wakati wa kuboresha jamii,” amesema  Hujjatul Islam Radmard.

Ameongeza kuwa maamurisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ambayo kwa bahati nzuri aghalabu ya Waislamu duniani wanayazingatia, ni maamurisho ya kipekee.

Amebaini kuwa maamurisho ya mwezi huu mtukufu yanamuelekeza Muislamu kujiboresha katika maisha kwa mujibu wa muongozo wa Mwenyezi Mungu SWT. Amesema huu ni mwezi wa kuwa na maadili mema, kuimarisha mawasiliano na wengine, kuonyesha ukarimu kwa mayatima na familia zisizojiweza. Aidha amesema huu ni mwezi wa kuhakikisha viungo vya mwili vinajiweka mbali na vitu vilivyoharamishwa.

3474503

captcha