Huku Waislamu wakiukaribisha mwezi wa Rabi-al-Awwal, mwezi ambao Mtume Muhammad (SAW) alizaliwa, baadhi ya mashirika na vikundi vya Kiislamu mjini Mumbai vimeanzisha kampeni mpya ya kueneza mafundisho na mahubiri ya Mtume Muhammad (SAW) kwa lengo la kuondoaa dhana potofu kuhusu Uislamu.
"Kampeni ya Mtume kwa Wote", inajumuishaa misikiti mbalimbali, madrasa, shule au vyuo vinavyoendeshwa na Waislamu, NGOs, mashirika ya kijamii na kitamaduni, na vyombo vingine vya Waislamu.
“Hili si zoezi la kiinjilisti. Tuna nia tu ya kufikisha ujumbe wa Mtume Muhammad SAW wa upendo, amani na udugu kwa ndugu zetu wote wasio Waislamu ili waweze kuwa na ufahamu bora wa Uislamu na wafuasi wake," kiongozi wa kampeni hiyo Yusuf Abrahani, ambaye pia ni Rais wa Islam Gymkhana, amesema.
Ubinadamu kwa Jumla
Kando na kubainisha kuwa ujumbe wa Mtume Muhammad (SAW) ni kwa wanadamu wote, kampeni hiyo itazingatia kutunza mazingira, kuhifadhi maji, huruma kwa masikini, wasiojiweza, mayatima, vibarua na wanawake.
"Kuna takriban misikiti 500 huko Mumbai, karibu shule 400 na vyuo 20 ... katika kampeni," alibaini Aamir Edresy, rais wa Chama cha Wanataaluma wa Kiislamu (AMP).
"Tunatuma maombi kupitia wanafunzi kwa familia zao kushiriki katika kampeni, kualika angalau wenyeji watano au majirani nyumbani kwao kwa chakula mnamo Oktoba 9, na kujaribu kufikisha ujumbe wa Mtume(SAW). Aidha kampeni pia itafanyika kwenye mitandao ya kijamii. ,” Edresy ameongeza
Qur’ani imejaa matukio mengi kuhusu sifa za kipekee za wa Mtume Muhammad (SAW), mojawapo ikiwa ni aya ifuatayo:
Qur’an inasema: “Na hatukukutuma wewe (Ewe Muhammad) ila uwe ni rehema kwa walimwengu wote.” Sura Al Anbiya-107.
Mapema mwaka huu, Baraza la Wazee wa Kiislamu lilianzisha kampeni mpya inayoangazia ujumbe wa wa Mtume Muhammad (SAW) uliojaa amani na upendo kwa binadamu.
Kampeni ya #Prophet_of_Humanity iliwashirikisha wanazuoni mbalimbali wakuu wa Kiislamu kuhusu ujumbe wa Mtume Muhammad (SAW) kwa ulimwengu.
3480644