IQNA

Waislamu wa Yemen

Wanazuoni wa Yemen wsisitiza haja ya kukuza Umoja wa Waislamu

19:22 - September 29, 2022
Habari ID: 3475854
TEHRAN (IQNA) – Wanazuoni wa Yemen wamesisitiza haja ya kuimarisha umoja wa Kiislamu, wakibainisha kwamba sikukuu ya kuzaliwa kwa Mtukufu Mtume (SAW) ni tukio la kukuza umoja.

Wasomi wa Yemen kutoka madhehebu mbali mbali za Kiislamu walizindua kongamano lao la kila mwaka katika mji mkuu Sana'a siku ya Jumatano.

"Masuala ya Wasiwasi na Matarajio ya Umma wa Kiislamu" ndiyo mada ya mkutano wa mwaka huu.

Akihutubia sherehe za ufunguzi, Abdul Majid al-Houthi, Mkuu wa Idara ya Wakfu ya Yemen, alisema mkutano huo umejadili masuala yote yanayohusiana na Umma wa Kiislamu.

Aidha amesisitiza umuhimu wa umoja na kusema wanazuoni wa Yemen wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa taifa katika masuala ya kulinda na kuendeleza umoja.

Abdul Majid al-Houthi pia walizikashifu baadhi ya taasisi za wanazuoni za ulimwengu wa Kiislamu ambazo zimenyamaza kimya mbele ya uvamizi na jinai zinazofanywa dhidi ya taifa la Yemen.

Sheikh Maher Hamoud, katibu mkuu wa Umoja wa Wanazuoni wa Mrengo wa Muqawama au Mapambano ya Kiislamu, pia alikuwa miongoni mwa wazungumzaji katika siku ya kwanza ya kongamano hilo.

Katika hotuba yake kwa njia ya video, Sheikh Hamoud alisema ingawa baadhi ya nchi za ulimwengu wa Kiislamu zimechagua kujisalimisha mbele ya mabeberu, mhimili wa muqawama unasimama dhidi ya uvamizi na vita vinavyoongozwa na Wazayuni na Marekani dhidi ya ulimwengu wa Kiislamu.

Pia aliisifu Yemen kama mfano bora wa mapambano ya Kiislamu dhidi ya mabeberu wavamizi na vikwazo.

Miongoni mwa masuala mengine yaliyoangaziwa katika hotuba za wanazuoni na maafisa katika siku ya kwanza ya mkusanyiko huo ni ulazima wa kufuata Siira ya Mtume Mtukufu Muhammad (SAW), upinzani wa kuanishwa uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni, kuendelea na mapambano ya kukomboa al- Quds Tukufu na Palestina nzima.

3480665

captcha