IQNA

Ukandamizaji Bahrain

Wapinzani Bahrain wataka utawala wa kifalme umuachilie mtetezi wa haki za binadamu

20:59 - December 02, 2022
Habari ID: 3476186
TEHRAN (IQNA) - Makundi ya upinzani Bahrain yamelaani mashtaka mapya dhidi ya mtetezi maarufu wa haki za binadamu na mwanaharakati wa kisiasa Abdulhadi al-Khawaja.

Khawaja ambaye tayari anatumikia kifungo cha maisha jela sasa anakabiliwa na mashtaka ya kuibua maandamano gerezani.

"Tunalaani vikali hukumu zilizotolewa na Mahakama ya Jinai na Mahakama ya Bahrain kwa misingi ya mashtaka mawili tofauti dhidi ya Abdulhadi al-Khawaja," ilisema taarifa ya Umoja wa Vijana wa Februari 14, ambayo ilichukua jina lake kutoka tarehe ambayo ulianza uasi dhidi ya ufalme wa kiimla unaotawala Bahrain

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, hukumu zilizotolewa dhidi ya mwanaharakati huyo wa miaka 61 ni kwa sababu ya msimamo wake wa kijasiri wa kuunga mkono haki za binadamu nchini Bahrain.

Umoja wa Vijana wa Februari 14 pia ulisema, "Utawala wa Al Khalifa unataka kuwaangamiza viongozi wa upinzani wa Bahrain kwa kutumia hukumu kali kama hizo na shutuma kali."

Kundi la upinzani lilimtaja Khawaja kama ngano ya uthabiti na uvumilivu.

Mwezi uliopita, msururu wa mashtaka mapya yalitolewa dhidi ya Khawaja, ambaye amefungwa kwa miaka 12 na kuteswa na kutelekezwa kiafya wakati akizuiliwa, jambo ambalo limemuacha na maumivu makali.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema yanaamini kuwa mashtaka hayo ni jaribio la kumtisha Khawaja na wafungwa wengine wanaolalamika wakiwa jela.

Miongoni mwa mashtaka mapya yaliyoletwa dhidi yake ni kuutusi utawala bandia wa Israel baada ya kuzungumza dhidi ya hatua ya watawala wa Bahrain kuanzisha uuhusiano wa kawaida na utawala huo unaoikalia kwa mabavu ardhi ya Palestina.

Khawaja, rais wa zamani na mwanzilishi mwenza wa Kituo cha Haki za Binadamu cha Bahrain (BCHR), alikamatwa na kufunguliwa mashtaka Aprili 9, 2011, kama sehemu ya kampeni ya ukandamizaji wa mamlaka ya Bahrain kufuatia maandamano ya kuunga mkono demokrasia katika nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi.. Ufalme wa Ghuba. Alihukumiwa Juni 22 mwaka huo, pamoja na wanaharakati wengine wanane, kifungo cha maisha.

Maandamano yamekuwa yakifanyika nchini Bahrain tokea mwezi Februari 2011. Wakati wananchi walipoanzisha mwamko dhidi ya ukoo  wa Aal Khalifa unaotawala nchi hiyo kwa mkono wa chuma.

Watu wanautaka utawala wa Aal Khalifa uachie madaraka na kuruhusu mfumo wa haki unaowawakilisha wananchi wote wa Bahrain uanzishwe.

3481490

captcha