IQNA

Wabeba silaha washambulia msikiti Nigeria, watu 11 wajeruhiwa

19:28 - December 03, 2022
Habari ID: 3476192
TEHRAN (IQNA) – Watu wenye silaha wameshambulia msikiti mmoja kusini mwa Nigeria siku ya Ijumaa wakijaribu kumteka nyara imamu bila kufanikiwa ambapo waliwafyatulia risasi na kwuajeruhi waumini kumi na mmoja.

Msikiti wa mji wa Ughelli, mji unaopatikana katika Jimbo la Delta, ulilengwa wakati wa sala ya asubuhi na watu wenye silaha. "Waumini kumi na moja wamejeruhiwa katika shambulio hili," msemaji wa Polisi wa Jimbo la Delta Bright Edafe amesema.

"Hadi sasa, hatujakamata mtu yeyote, lakini niwakuhakikishia kuwa tutawakamata waliohusika na shambulio hili," ameongeza.

Vyombo vya habari vya eneo hilo, vikimnukuu kiongozi wa jamii na mmoja wa waliojeruhiwa, vinaripoti kwamba mmoja wa maimamu alitekwa nyara na washambuliaji. Lakini polisi walikanusha habari hii, na kuongeza: "Ilikuwa nia yao kumkamata, lakini hawakufanikiwa". Sababu hasa za shambulio hili bado hazijajulikana.

Visa vya utekaji nyara hutokea mara kwa mara katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika, iliyokumbwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi na kukabiliwa na ukosefu wa usalama wa jumla, kati ya mashambulizi ya wahalifu na makundi ya kijihadi.

Wasiwasi umetanda Nigeria wakati ambapo wapiga watashiriki katika uchaguzi  mnamo Februari 25 mwakani kumchagua mrithi wa Rais Muhammadu Buhari, ambaye anaachia ngazi baada ya mihula miwili, kama ilivyoainishwa katika katiba.

3481496

Kishikizo: nigeria msikiti
captcha