IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Nusu fainali ya Mashindano ya Qur'ani ya Kituo cha Dar-ul-Quran cha Iran Yaanza

22:02 - December 05, 2022
Habari ID: 3476201
TEHRAN (IQNA) - Duru ya nusu fainali ya mashindano ya nchi nzima ya Qur'ani yaliyoandaliwa na Kituo cha Dar-ul-Quran cha Imam Ali (AS) nchini Iran inaendelea.

Hili ni toleo la 16 la mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka na kituo cha wanaharakati wa Qur'ani kote nchini ili kukuza ujfunzaji wa Qur'ani na kutambua vipaji vya Qur'ani.

Washindani wanashindana katika kategoria za qiraa, tarteel, na kuhifadhi Qur’ani Tukufu (katika viwango tofauti).

Wale wa kategoria za qiraa na tarteel hutuma faili zilizorekodiwa za usomaji wao kwa kamati ya maandalizi na jopo la waamuzi litachagua wale ambao wataingia fainali kulingana na utendaji wao kwa suala la Lahn, Sawt, Tajweed, Waqf  na Ibtida.

Wataalamu 19 wa Qur'ani katika sehemu ya wanaume na wataalamu 22 wa Qur'ani katika sehemu ya wanawake wanahudumu kama wajumbe wa jopo la wasuluhishi.

Majina ya watakaofuzu kwa fainali hizo yatatangazwa na kituo hicho Jumanne, Desemba 13.

 4104343

captcha