IQNA

Mashindano ya 39 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran: Awamu ya Awali ya Kitengo cha Wanaume

MASHHAD (IQNA) - Awamu ya awali ya kategoria za wanaume katika Mashindano ya 39 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran ilianza Jumapili mjini Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran

Jopo la majaji katika duru hii ya mchujo linapitia klipu zilizorekodiwa na kutumwa na washiriki  kutoka nchi mbali mbali duniani na baada ya hapo  litachagua wagombeaji wakuu kwa hatua ya fainali itakayoanza Februari 18.