IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran: IRGC ni nguzo na msingi wa nguvu za Jamhuri ya Kiislamu

18:46 - January 20, 2023
Habari ID: 3476434
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ni nguzo muhimu na ni msingi wa nguvu za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kuwa, wananchi na fikra za kitawhidi za maimamu wawili wa Mapinduzi ya Kiislamu, daima zimekuwa ndizo ngao za jeshi la IRGC.

Hujjatul Islam Walmuslimin Haj Ali Akbari amesema hayo kwenye khutba za sala hiyo na kuzungumzia pia kukaribia kuingia Waislamu kwenye mwezi mtukufu wa Rajab akisisitiza kuwa, ni neema ya Mwenyezi Mungu kuweza Muislamu kuingia kwenye miezi mitukufu kama wa Rajab.

Amesema, ni neema kubwa sana pia kuweza Waislamu kupata fursa ya kuangaziwa na nuru kama hiyo katika dunia hii iliyojaa kiza na uchafu wa kila namna na moja ya fursa hizo ni miezi ya Rajab, Shaaban na Ramadhan na hasa usiku wenye cheo yaani Laylatul Qadr.

Khatibu huyo wa muda wa Sala ya Ijumaa ya Tehran vile vile amegusia kitendo cha Bunge la Ulaya cha kuliweka jina la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC kwenye orodha ya kile kinachodaiwa kuwa eti ni makundi ya kigaidi na mbali na kulaani hatua hiyo amesema, wananchi na fikra za kitawhidi za maimamu wawili wa Mapinduzi ya Kiislamu, daima zimekuwa ndizo ngao za jeshi la IRGC.

Hujjatul Islam Walmuslimin Haj Ali Akbari vile vile amesema, njama za maadui ni kubwa na ni za kila upande lakini muda wote mahesabu yao ni mabovu. Amesema, mahesabu ya adui yanategemea vitu vya kimaada, vya kuonekana kwa macho na vya kushikika kwa mkono wakati moja ya nguvu muhimu za Jamhuri ya Kiislamu ni taufiki na ulinzi wa Mwenyezi Mungu na ni imani iliyokita mizizi ya taifa la Iran pamoja na kuwepo kiongozi mwenye hikma na busara kubwa, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.

4115883

captcha