IQNA

Wasomaji Maarufu wa Qur'ani Tukufu /21

Qari aliyekuwa maarufu miongoni mwa wanasiasa wa Misri

18:31 - January 23, 2023
Habari ID: 3476452
TEHRAN (IQNA) – Ustadh Taha al-Fashni alikuwa qari maarufu wa Qur'ani Tukufu na msomaji Ibtihal nchinia Misri ambaye alikuwa na wafuasi wengi sio tu miongoni mwa Waislamu bali pia wasio Waislamu.

Visomo vyake vilikuwa vya kuvutia sana hivi kwamba alijulikana hata na viongozi wakuu wa kisiasa wa Misri.

Ustadh Taha Musa Hassan, ambaye alikuwa maarufu kama Taha al-Fashni, alizaliwa mwaka wa 1900 MIladia katika mji wa Fashn katika Jimbo la Beni Suef la nchi ya Kiarabu.

Alifuata nyayo za Sheikh Ali Mahmoud katika Ibtihal (kisomo cha dua). Katika usomaji wa Qur'ani Tukufu, alikuwa akipenda sana kufuata mtindo wa Sheikh Mustafa Ismail.

Miongoni mwa kazi zake kuu za Ibtihal ni Hubb al-Hussein (AS), Ya Ayuhha al-Mukhtar, na Milad Taha. Aliaga dunia mnamo 1971.

Kulikuwa na wasomaji wakubwa wa Ibtihal kabla ya Taha al-Fashni, kama vile Ali Mahmoud na Syed Darwish, lakini wakati wa uhai wake, maendeleo katika utayarishaji wa ala za kurekodi sauti iliruhusu maonyesho yake kufikia wasikilizaji wengi zaidi na kwa ubora.

Utendaji wa nguvu wa Taha al-Fashni uliathiri kila mtu. Hata viongozi wa ngazi za juu nchini Misri marais Gamal Abdel Nasser na Anwar Sadat walipenda kazi zake.

Mojawapo ya kazi zake bora zaidi ilikuwa Hubb al-Hussein (AS) ambayo iliwavutia Wakristo kwenye sanaa ya Ibtihal na kuwafanya wawe na hamu ya kujifunza kuhusu watu muhimu katika historia ya Uislamu.

Al-Fashni alipata fursa ya kujishughulisha katika fani ya muziki na kupata pesa nyingi lakini alichagua fani ya Ibtihal na kusoma kasida za kumsifu Mtukufu Mtume (SAW) na Ahl-ul-Bayt (AS).

Ifuatayo ni klipu zamani inayoonyesha qari huyu mashuhuri akisoma aya za 185-200 za Surah Al-Imran:

captcha