IQNA

Tafsiri na Wafasiri wa Qur'ani Tukufu /15

Tafsiri ya Qur’ani Tukufu ya Mulla Sadra, Mwanafalsafa Mwislamu

22:15 - January 25, 2023
Habari ID: 3476460
TEHRAN (IQNA) – Tafsir al-Quran al-Karim ni tafsiri ya Qur’ani Tukufu iliyoandikwa na Mulla Sadra, mwanafalsafa mashuhuri wa ulimwengu wa Kiislamu na mwanzilishi wa chuo cha Hikma al-Muta’aliya.

Tafsiri hiyo imeandikwa kwa Kiarabu na ambapo mwandishi amezifasiri aya kwa matazamo wa kifalsafa na kiirfan.

Ṣadr ad-Din Muhammad Shirazi (1571-1640 Miladia), ambaye ni maarufu zaidi kama Mulla Sadra, alikuwa mwanairfani wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia Ithnaasharia na halikadhalika alibobea katika utaalamu wa Uislamu na falsafa na hivyo akawa mwanzilisi wa chuo cha Hikma al-Muta'aliya.

Aliishi katika miji ya Shiraz, Qazvin, Isfahan na Qom nchini Iran kabla ya kuhamia katika kijiji kiitwacho Kahak, karibu na Qom, aliko ishi hadi miaka ya mwisho ya maisha yake.

Amearifisha mfumo wake wa kifalsafa katika kitabu Asfar al-Arba’a (safari nne). Alikuwa na umilisi katika nyanja mbalimbali za maarifa lakini alihusika zaidi katika falsafa.

Tafsir al-Quran al-Karim na Sharh Usul al-Kafi ni miongoni mwa vitabu vyake muhimu.

 

Mbinu ya Ufasiri wa Qur’ani Tukufu

Katika Tafsir al-Quran al-Karim, Mulla Sadra anatanguliza njia nne za kawaida za kufasiri, akiita moja wapo njia ya “wale walio imara katika elimu”, ambayo ni njia ile ile inayotumiwa na Mitume wa Mwenyezi Mungu na Ahl-ul-Bayt (AS) katika kuifahamu Qur’ani  Tukufu. Anasema njia hii ni kwa wale waliochaguliwa na Mwenyezi Mungu kugundua ukweli, maana za kiroho, siri za irfan na ishara za Wahyi.

Anaongeza kuwa, katika kugundua maana maalum au ishara kutoka kwa Mwenyezi Munguc, wao kamwe hawadhoofishi maana dhahiri na wala hawavurugi maana  ya siri.

Mulla Sadra anaichukulia njia hii kuwa njia pekee ya kina ya kuelewa na kupata maana iliyofichika ya Qur’ani Tukufu, ambayo haiwezi kupatikana kupitia kanuni za kisarufi za Kiarabu na maana za maneno kwa sababu kama hilo lingewezekana, wasomi wote wa lugha ya Kiarabu wangeweza kufichua siri za Qur’ani Tukufu.

Anaamini kwamba njia muhimu na ya kutegemewa ya tafsiri ni ile njia angavu inayotokana na nuru ya utume na Uimamu.

Anachukulia maarifa angavu kuwa njia bora na yenye thamani zaidi ya utambuzi na njia ya kufikia wokovu.

 Vipengele katika tafsiri ya Qur’ani ya Mulla Sadra

Mulla Sadra mara nyingi huanza tafsiri ya kila aya kwa mjadala wa maneno na kutoa maoni tofauti ya wanachuoni kuhusu neno au kifungu cha maneno katika aya hiyo, bila kupingana maoni hayo. Wakati mwingine huenda zaidi na kujaribu kuonyesha ubora wa moja ya maoni.

Anatilia maanani zaidi usomaji wa Kufi na Basri wa Qur’ani Tukufu na anataja maoni kutoka kwa baadhi ya watu kama Nakhaei, Qatada na Hassan Basri na kisha anazungumzia Sha’an Nuzul (sababu ya kuteremshwa) ya aya hiyo.

Pia anajadili maneno magumu na kisha kulingana na mtazamo wake wa irfani, hutoa tafsiri yake.

Mulla Sadra anaifasiri Qur’ani kwa kutumia Qur’ani. Aidha, anataja tafsiri za wengine iwapo anakubaliana nazo au la.

Tafsiri za tafsiri zake za baadhi ya Sura za Qur’ani kama vile Sura Al-Waqi’a, Al-Jumu’a, Triq, Al-A’ala na Noor zimechapishwa kwa lugha ya Kifarsi au Kiajemi.

captcha