IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Wanaovunjia heshima Qur'ani Tukufu wanaoungwa mkono na nchi za Magharibi

16:45 - January 27, 2023
Habari ID: 3476470
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema serikali za Magharibi zinaunga mkono kuvunjiwa heshima dini za Mwenyezi Mungu hususan Uislamu.

Hujjat-ul-Islam wa Muslimin Kazem Siddiqui, imamu wa muda wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran katika khutba zake ameashiria vitendo vya hivi karibuni vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu na kusema kuwa, ulimwengu wa makafiri unauogopa Uislamu na ulimwengu wa Magharibi una wasiwasi juu ya mvuto wa Uislamu. 

Aidha amesema: "Serikali za Magharibi zinaunga mkono kuvunjiwa heshima dini za Mwenyezi Mungu hususan Uislamu na vitendo hivyo si kazi ya jarida pekee. Serikali zote za magharibi zinapokezana katika mwelekeo huu na unaendelea, lakini wamesahau aya ya Qur'ani Tukufu isemayo; "… Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu..." (Sura Ibrahim aya ya 42)

Hujjat-ul-Islam wa Muslimin Kazem Siddiqui, amegusia pia vikwazo vya Wamagharibi dhidi ya Iran na kusema moja ya taasisi zilizolengwa ni Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC). Ameongeza kuwa, jeshi hilo limejitolea kwa ajili ya dini, mapinduzi, watu na nchi tangu kuasisiwa kwake.

Khatibu Sala ya Ijumaa aliongeza kuwa: "IRGC pia imehudumia watu wa Ulaya kwa sababu Luteni Jenerali Shahidi Qassem Soleimani, kwa ubunifu wake na  kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu, aliweza kuunda harakati ya Mujahidina na kupigana na  kundi la kigaidi la Daesh au ISIS, ambalo liliundwa na nchi za Ulaya na Marekani, na hivyo IRGC ilizuia moto wa Daesh kufika Ulaya."

Halikadhalika amesema madola ya Magharibi yanataka  IRGC iwe dhaifu, lakini IRGC itaimarika zaidi na madola hayo yatafedheheka.

4117546

captcha