IQNA

Wasomaji Maarufu wa Qur'ani Tukufu /23

Shahat Muhammad Anwar; Qari aliyekuwa Mwalimu wa Qur'ani utotoni

18:02 - January 27, 2023
Habari ID: 3476473
TEHRAN (IQNA) – Shahat Muhammad Anwar alikuwa mmoja wa wasomaji mashuhuri wa Qur’ani Tukufu nchini Misri ambaye alipata umaarufu katika umri mdogo kwa sababu ya kipaji chake katika fani hii.

Ustadi wake wa usomaji wa Qur'ani ulikuwa kwamba alijulikana kama Ustadh katika utoto wa mapema.

Shahat alizaliwa Julai 1950 katika kijiji cha Kafr el-Wazir katika Jimbo la Dakahlia nchini Misri. Alimpoteza baba yake alipokuwa na umri wa miezi mitatu.

Anwar alianza kujifunza Qur'ani Tukufu akiwa na umri mdogo na akaihifadhi kikamilifu  akiwa na miaka 8. Alipokuwa na umri wa miaka kumi, ami yake alimpeleka katika kijiji cha Kafr el-Maqam ili kujifunza usomaji wa Tajweed kwa Ustadh Seyed Ahmed Fararahi.

Alijifunza usomaji wa Qur'ani Tukufu na punde akawa qari maarufu.

Wasomaji bingwa wa Qur'ani Tukufui kama Said Abdul Samad al-Zanani na Hamdi Zamil walikuwa miongoni mwa wale walioanza njia ya usomaji wa Qur'ani baada ya kuhudhuria duru za usomaji Qur'ani za Shahat.

"Kwa kuhifadhi Qur'ani (katika utoto), nilihisi nimefikia furaha isiyoelezeka," alisema. "Baada ya hapo, kwa sababu nilikuwa na sauti nzuri na Lahn yangu ilikuwa kama ile ya maustadhi wakubwa, ... nilijulikana kama "Ustadh mdogo".

Kisha akaalikwa kusoma Quran katika kipindi ambacho kilihudhuriwa pia na Kamil al-Balouhi, mkuu wa Redio ya Qur'ani ya Misri wakati huo.

Al-Balouhi alimwalika asome Qur'ani kwenye Redio na hivyo alijiunga na Idhaa ya Qur'ani ya Misri mnamo 1979.

Shahat Muhammad Anwar alisafiri katika nchi nyingi kama Hispania, Ufaransa, Marekani, Nigeria, Cameroon, Argentina, na Uingereza, kwa ajili ya usomaji wa Qur'ani.

Wanawe watatu na mabanati sita wote ni wahifadhi wa Qur'ani Tukufu. Wanawe Anwar na Mahmoud pia ni miongoni mwa maqari mashuhuri.

Kwa sababu ya ugonjwa wa ini, hakuweza kusoma Qur'ani katika miaka minne ya mwisho ya maisha yake.

Shahat alirejea kwa Mola wake Januari 13, 2007 akiwa na umri wa miaka 57 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Ifuatayo ni qiraaa yake ya Surah Al-Fatiha:

captcha