IQNA

Wasomaji Maarufu wa Qur'ani Tukufu /24

Shaban Abdul Aziz Sayyad; Qari aliyekuwa na visomo vyenye mvuto na mashuhuri

18:23 - January 29, 2023
Habari ID: 3476482
TEHRAN (IQNA) – Shaban Abdul Aziz Sayyad alikuwa miongoni mwa makari mashuhuri wa Misri ambaye alisoma Qur’ani kwa shauku na usomaji wake ulikuwa maarufu sana.

Shaban Sayyad alizaliwa Septemba 20, 1940, katika kijiji cha Sarawak katika Jimbo la Menofia nchini Misri.

Baba yake, Abdul Aziz Esmail Sayyad alikuwa qari anayejulikana wakati huo na hii ilitosha kwa kijana Shaban Sayyad kukuza hamu kubwa ya usomaji wa Qur'ani Tukufu.

Alikamilisha kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka saba. Kisha akajifunza ujuzi wa kusoma na Tajweed, na akiwa na umri wa miaka 12, tayari alikuwa akipokea mialiko ya kushiriki katika duru za Qur'ani Tukufu.

Baada ya kupokea diploma yake ya shule ya upili, Shaban aliingia kitivo cha Osoul El Dine katika Chuo Kikuu cha Al Azhar na kusoma falsafa.

Sayyad alifuata mitindo ya usomaji ya mabwana wakubwa kama Sheikh Muhammad Rifat na Sheikh Mustafa Ismail.

Mnamo mwaka wa 1975, qari wa juu aliweza kuingia kwa mafanikio katika Idhaa ya Qur'ani ya Misri na huu ulikuwa mwanzo wa utangazaji wa kisomo chake, na kumfanya kuwa maarufu zaidi nchini kote na katika ulimwengu wa Kiislamu.

Alisoma Qur'ani Tukufu katika misikiti mikubwa na maarufu ya Misri, kama vile Msikiti wa Al-Hussein (AS) na Msikiti wa Al-Sayeda Zainab (SA) huko Cairo.

Wakati wa uhai wake, alisafiri katika nchi nyingi, ikiwa ni pamoja na Kuwait, Jordan, Iran, Umoja wa Falme za Kiarabu, Syria, Iraq, Marekani, Uingereza, Ufaransa na Indonesia, akitoa kumbukumbu muhimu kwa watazamaji kutoka mataifa mbalimbali.

Wakati mmoja Shaban Sayyad, Mustafa Ghalwash na Mohamed Mahmoud Tiblawi walikwenda Kuwait na kusoma Qur'ani kwa mwezi mmoja huko katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Shaban Sayyad alifuata mtindo maarufu, kumaanisha kwamba usomaji wake ulikaribishwa kwa shauku na wenyeji wa Misri. Mtindo huu pia ulileta shauku iliyoathiri hadhira.

Mbali na qiraa ya Qur'ani, ingawa hakukubali nafasi rasmi katika Al-Azhar, alifundisha masomo juu ya tafsiri ya Qur'an, ufahamu wa Qur'ani na Hadithi.

Shaban Sayyad alifariki mwaka 1998 akiwa na umri wa miaka 58.

Ifuatayo ni kisomo chake cha Aya ya 32 ya Surah Al-Furqan:

Habari zinazohusiana
captcha