IQNA

Udharura wa kudumisha umoja wa Waislamu

14:26 - July 30, 2015
Habari ID: 3336969
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu amesisitiza udharura wa kudumishwa umoja wa Waislamu kwa ajili ya kutatua matatizo ya Mashariki ya Kati.

Ayatullah Mohsen Araki alisema hayo Jumanne  mwishoni mwa siku ya kwanza ya mkutano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Maulama wa Muqawama unaofanyika Beirut Lebanon ambapo aliashiria pia mgogoro wa Syria na kusema, njia sahihi ni kudumishwa umoja na amani baina ya makundi yote ya Kiislamu. Ayatullah Araki amesema kuwa, nchi zote za Kiislamu zinapaswa kukusanya nguvu zao kwa ajili ya umoja wa Umma wa Kiislamu na kwamba, Uturuki nayo badala ya kuishambulia Syria inaweza kushiriki katika juhudi za utatuzi wa kisiasa wa mgogoro wa nchi hiyo ya Kiarabu. Ayatullah Araki amesema, hatua ya Uturuki ya kuyaunga mkono makundi ya kigaidi na kushambulia ardhi ya Syria haitakuwa na matokeo mengine ghairi ya hasara kwa nchi hiyo, kama ambavyo Saudi Arabia itapata hasara kwa kuishambulia kwake Yemen.
Mkutano wa kwanza wa siku mbili wa "Jumuiya ya Kimataifa ya Maulama wa Muqawama" wenye anwani ya "Umoja Kwa Ajili ya Palestina na Kuiangamiza Israel" ulianza jana mjini Beirut Lebanon ukihudhuriwa na zaidi ya maulama na wanafikra 150 wa madhehebu mbalimbali ya Kiislamu na shakhsia wa ulimwengu wa Kiislamu kutoka zaidi ya nchi 65 duniani.../mh

3336271

captcha