IQNA

Sisitizo la Al Azhar kuhusu Umoja baina ya Shia na Suni

16:58 - August 18, 2015
Habari ID: 3345811
Mhadhiri mmoja wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar nchini Misri amesema kuwa, hakuna tatizo lolote katika kuwakurubisha pamoja Waislamu wa madhehebu ya Suni na Shia.

Sheikh Ahmad Karimah, mmoja wa wahadhiri katika chuo hicho, amesema kuwa kile kinachoukumba ulimwengu wa Kiislamu hii leo ni kuibuliwa tofauti baina ya Waislamu na madhehebu za Kiislamu. Alimu huyo ametoa wito kwa wafuasi wa dini ya Kiislamu kushikamana na itikadi kuu zinazowaunganisha pamoja na kutotoa mwanya kwa makundi ambayo yanafanya njama za kuibua farqa baina yao. Sheikh Ahmad Karimah amemtaja Sheikh Muhammad Shaltut na masheikh wengine wa zamani wa al-Azhar, kuwa miongoni mwa maulama wakubwa wa Kisuni waliokuwa wakihimiza sana umoja baina ya Masuni na Mashia, na kuongeza kuwa hivi sasa hakuna tatizo lolote juu ya suala hilo. Si vibaya kuashiria hapa kuwa, magaidi wa Kiwahabi na Kisalafi ndio wamekuwa wakiendesha kampeni ya kuibua tofauti baina ya umma wa Kiislamu kwa kuwataja wale ambao hawafuati mienendo yao kuwa ni makafiri na hivyo kuhalalisha umwagaji wa damu yao.../mh

3345610

captcha