Kwa mujibu wa taarifa, msaada wa Ozil, ametoa mchango huo ambao utatumika kununua futari kwa ajili ya watu 16,000 nchini Uturuki na Syria katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Aidha fedha hizo pia zitatumika kununua vifurishi 90,000 vya futari katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Mkuu wa Shirika la Hilali Nyekundu ya Uturuki Kerem Kinin amemshukuru mchezaji soka huyo na amemhakikishia kuwa misaada hiyo itawafikia wanaohitaji haraka iwezekanavyo.
Ozil, ambaye ni raia wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki, ni kati ya wachezaji wanaolipwa kitita kikubwa zaidi katika timu ya Arsenal. Ozil ni Mwislamu anayefungamana na mafundisho ya Kiislamu na huwasaidia maelefu ya watoto wanaohitaji matababu huku akitoa msaada wa chakula kwa makumi ya maelfu ya familia kila mwaka.
3471341