IQNA

Aya za Machipuo/ 1

Usomaji wa aya ya Bishara ya Rahma kwa sauti ya Ustadh Abdul Aziz Sayad

TEHRAN (IQNA)- Kwa mnasaba wa kuwasili kwa siku Nowruz ambazo ni maadhimisho ya kuwadia mwaka mpya wa Kiirani wa Hijria Shamsia sambamba na kuanza msimu wa machipuo na kuhuishwa ardhi, IQNA inasambaza aya za Qur’ani Tukufu zinazoashiria machipuo kwa sauti za wasomaji maarufu wa Qur’ani Tukufu katika Ulimwengu Kiislamu. Katika sehemu ya kwanza, tumewaandalia qiraa ya Aya ya 48 ya Surah Al-Furqan kwa sauti ya Ustadh Shaban Abdulaziz Sayad wa Misri.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ
وَهُوَ الَّذِي أَرْسَلَ الرِّيَاحَ بُشْرًا بَيْنَ يَدَيْ رَحْمَتِهِ وَأَنْزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً طَهُورًا 

Naye ndiye anaye zituma pepo kuwa bishara njema kabla ya rehema yake, na tunayateremsha kutoka mbinguni maji safi.