IQNA

Kitabu Kinachoongoza Waongofu Kwenye Ulimwengu wa Kiislamu

11:48 - October 11, 2023
Habari ID: 3477713
TEHRAN (IQNA) – Rehema ya Mwenyezi Mungu husaidia kuleta msamaha kwa mwanadamu katika dunia hii au ijayo ili asiungue katika moto wa jahannam.

Moja ya dalili za rehema hii ni Shifa’a kuomba kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Shifaa ni nini na ni nani anayeweza kutufanyia Shifaa?

Kutokana na kanuni ya hiari, mwanadamu wakati mwingine anaweza kufanya makosa katika uchaguzi wake na kuchagua njia ya dhambi Ili kufidia, mtu anatakiwa kujutia dhambi na kutubia kwake  Kwa hiyo Toba yani kutubu na kurejea katika njia yaMwenyezi  Mungu humsaidia mtu kupokea Shifaa.

Shifa’a maana yake ni kuomba kitu kutoka kwa mwenye kufanya maombi,  Mtume Muhammad (s.a.w) au wengineo Shifa’a  wanamuomba Mwenyezi Mungu na kumuomba awasamehe watenda dhambi au anyanyue hadhi ya mtu.

Imani katika Shifa’a ni kizuizi chenye nguvu ambacho kinasimama katika njia ya mafuriko makubwa ya dhambi, Mwenye kuamini Shifa’a, anaitaka na anajua kwamba ni lazima awe mwangalifu juu ya anayoyasema na kuyatenda na kuepuka madhambi ili aweze kuyapokea.

Shifa’a ni fundisho linalomsaidia mtu kukua na kurejea kutoka kwenye njia ya dhambi na kuzuia kupoteza matumaini.

Katika Uislamu wa Shia, imani katika Shifa’a ni muhimu, Imamu Sadiq (AS) alisema; Yeyote atayekanusha mambo matatu, yaani Mi’raj, kuswali na kujibu kaburini, na Shifa’a, si miongoni mwa Mashia  na wafuasi wetu.

Imani ya Shifa’a ina athari nyingi chanya, zikiwemo zifuatazo;

  • Matumaini ya kupata msamaha, Kuamini Shifa’a humsaidia mtenda dhambi kuwa na matumaini kwamba atasamehewa kwa kupata ridhaa ya mwenyezi Mungu.

Bahari Ambayo Kina Chake Hauwezi Kushikana

2- Kuhimizwa kutimiza faradhi za kidini, Aliyetenda madhambi atatubu na atafanya juhudi za kuvuta rehema na msamaha wa Mwenyezi Mungu.

3- Kutarajia malipo, Mwenyezi Mungu ameahidi baraka za milele kwa waja wake na akawahimiza waja walioasi watubu, Kwa kuzingatia kanuni ya kukubali toba, Shifa’a ni malipo ya Mwenyezi Mungu kwa wale wanaotubu.

Sasa swali ni nani atafanya Shifa’a?

1- Mwenyezi  Mungu

Mwenyezi Mungu anasema; Wa mwisho kufanya Shifa’a ni  Mwenyezi Mungu, ambaye ni Mwingi wa Rehema na Mwenye kurehemu.

2- Manabii wa Mwenyezi Mungu

Kwa mujibu wa Qur'ani Tukufu, Mtume Muhammad (S.A.W) anapomwombea msamaha mtu, Mwenyezi Mungu huipokea sala hiyo na humsamehe mtu .

“Hatukutuma Mitume yoyote kwa sababu yoyote isipokuwa kutiiwa kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Na lau wakijidhulumu nafsi zao na wakakujia wewe  Mtume Muhammad (S.A.W) wakiomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu, na kama Mtume naye angewaombea msamaha kwa Mwenyezi Mungu, bila shaka wangemkuta Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu tafsiri ya aya ya 64 ya Sura An-Nisa.

Kuna Hadithi ambayo kwa hayo  makundi matatu yanaweza kufanya Shifa’a kwa watu mbele ya Mwenyezi Mungu, Mitume, wanachuoni wa kidini na mashahidi.

3- Qur’ani Tukufu

Kwa mujibu wa Imam Ali (AS) katika Khutba ya 176 ya Nahj al-Balagha, Qu’rani ni “mwombezi na uombezi wake utakubaliwa, na ni mzungumzaji anayeshuhudiwa.

Kwa hiyo, kukimbilia katika Qur'ani Tukufu na kuyafanyia kazi mafundisho yake kutamsaidia mtu kupata uongofu katika ulimwengu huu na ujao.

 

3485504

 

 

captcha