IQNA

Hamas yataka Usitishaji vita uendane na kuondoa mzingiro Gaza

18:30 - August 11, 2014
Habari ID: 1438342
Khalid Mashal Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina Hamas amesema kuwa, usitishaji wowote wa vita unapaswa kufungamana na uondoshwaji mzingiro wa kidhuluma uliowekwa dhidi ya wananchi wa Ghaza.

Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kufikiwa makubaliano mapya ya usitishaji vita kwa muda wa masaa 72 kati ya utawala wa Kizayuni wa Israel na makundi ya Kipalestina yanayopambana na utawala huo ghasibu, Khalid Mash al amesisitiza kwamba, moja kati ya  mambo yanayofuatiliwa ni kuhakikisha kwamba misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula na madawa inafikishwa kwa wananchi wa Ghaza. Kiongozi huyo wa Hamas ameongeza kuwa, lengo lingine la Wapalestina ni kuhakikisha kwamba mzingiro wa kidhulma dhidi ya wananchi wa Ghaza unaondolewa. Ameongeza kuwa, wanamuqawama wa Kipalestina wako tayari kuendelea na mapambano dhidi ya Wazayuni, iwapo utawala huo ghasibu utaendeleza mashambulio dhidi ya wananchi wa Ghaza. Inafaa kuashiria hapa kuwa, zaidi ya Wapalestina 1,920 wameuawa shahidi na wengine wanaokaribia 10,000 kujeruhiwa, tokea Israel ilipoanzisha mashambulio dhidi ya Ghaza tarehe 8 mwezi uliopita.

1437987

Kishikizo: ghaza hamas wazayuni
captcha