IQNA

Mauaji ya Kimbari Gaza

UNRWA yaomba misaada ya kibinadamu Palestina, Israel yaendeleza mauaji ya kimbari

17:02 - April 25, 2024
Habari ID: 3478731
IQNA - Ili kushughulikia mahitaji ya dharura zaidi ya Wapalestina huko Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limewasilisha ombi la dharura la msaada wa  dola bilioni 1.21.

"Makovu ya vita yanaonekana kwa kiwango kikubwa huko Gaza. Wakati huo huo, ghasia zinaongezeka katika Ukingo wa Magharibi,” Kamishna Mkuu wa UNRWA Philippe Lazzarini alisema katika taarifa yake.

"Ni muhimu kuunga mkono UNRWA katika kutoa msaada wa kuokoa maisha wa kibinadamu na huduma za maendeleo katika afya na elimu," aliongeza.

UNRWA imesema ombi hilo linalenga kujibu mahitaji ya dharura zaidi ya Wapalestina milioni 1.7 katika Ukanda wa Gaza na zaidi ya wakimbizi 200,000 katika Ukingo wa Magharibi, ikiwa ni pamoja na Jerusalem Mashariki al-Quds.

"Miezi iliyopita ilithibitisha kuwa hakuna mbadala au mbadala wa UNRWA," Lazzarini aliongeza.

Utawala dhalimu wa Israel ulianza vita vya mauaji wa kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza Oktoba 7, 2023.

Zaidi ya Wapalestina 34,200 wameuawa shahidi tangu wakati huo na wengine 77,200 kujeruhiwa katika mzingiro mkali uliowekwa na Israel, ambao uliwaacha wakaazi wote, haswa wakaazi wa kaskazini mwa Gaza, kwenye hatihati ya njaa.

Zaidi ya miezi sita baada ya vita vya Israel, maeneo makubwa ya Gaza sasa ni magofu, huku 85% ya wakazi wa eneo hilo wakiwa wakimbizi wa ndani katika eneo hilo ambalo limezingirwa na kusababisha uhaba mkubwa wa  chakula, maji safi na dawa, kulingana na UN.

Mwezi Machi, Umoja wa Mataifa ulionya juu ya "njaa inayokaribia" huko Gaza na kuomba hatua za haraka kuzuia maafa ya kibinadamu katika eneo hilo.

UNRWA iliundwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa zaidi ya miaka 70 iliyopita ili kuwasaidia Wapalestina waliofurushwa kwa nguvu kutoka katika ardhi yao ambayo ilinyakuliwa na Wazayuni ambao waliunda utawala haramu wa Israel.

Shirika hilo linatoa msaada muhimu kwa mamilioni ya wakimbizi wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza, Ukingo wa Magharibi, Jordan, Lebanon, Syria, na maeneo mengine ambako idadi kubwa ya Wapalestina waliosajiliwa wanaishi.

Afrika Kusini ilifungua kesi dhidi ya utawala wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ikiutuhumu utawala huo kuwa unatekeleza mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza. Uamuzi wa muda wa mwezi Januari uliiamuru Israel  kusitisha vitendo vya mauaji ya halaiki na kuchukua hatua za kuhakikisha kwamba msaada wa kibinadamu unatolewa kwa raia huko Gaza. Israel ilipuuza uamuzi huo.

3488078

Habari zinazohusiana
captcha