Hatahivyo mbali na madirisha kuvunjwa hakuna hasara iliyopatikana katika hujuma hiyo.
Wasimamizi wa msikiti huo wamesema watawasilisha lalalmiko ramsi dhidi ya aliyetekeelza hujuma hiyo inagawa utambulisho wake haujaweza kubainika.
Waislamu nchini Uholanzi wameingiwa na wasi wasi kutokana na misikiti kulengwa na wenye chuki dhidi ya Uislamu katika miezi ya hivi karibuni na wametaka polisi nchini humo kuhakikisha maeneo ya ibada ni salama.
Hivi karibuni pia Msikiti wa Jamia wa Utrecht nchini Uholanzi ulishambuliwa na watu wasiojulikana.
Mashambulizi kama hayo yamepelekea wasio wasio kuongezeka miongoni mwa Waislamu.