IQNA

Pakistan yatangaza maelekezo ya kufuatwa Mwezi wa Ramadhani kuzuia kuenea COVID-19

16:31 - April 04, 2021
Habari ID: 3473782
TEHRAN (IQNA) –Pakistan imetangaza maelekezo ya kufuatwa na Waislamu misikitini katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili kuzuia kuenea corona au COVID-19.

Katika taarifa  Kamati ya Kitaifa ya Kupambana na Corona nchini Pakistan imesema baada ya mashauriano na Maulamaa nchini humo imeamuliwa kuwa Sala ya Tarawih misikitini na ibada zinginezo za Mwezi wa Ramadhani ambazo hufanyika katika kumbi za kidini maarufu kama Imambargah zifanyike kwa kuzingatia kanuni za kiafya za kuzuia kuenea COVID-19.

Wasimamizi wa misikiti na Imambargah wamepewa idhini ya kuendesha ibada kwa sharti la kuzingatia kanunui za kuzuia kuenea COVID-19.

Taarifa hiyo imesema iwapo itahisika kanuni hizo hazizingatiwi au idadi ya maambukizi imeongezeka, basi agizo la utumizi wa maeneo hayo ya ibada litaangaliwa upya.

Kwa mujibu wa maagizho hayo hakuna ruhusua ya kutumia mikeka na mazulia ya umma katika Misikiti au Imambargah na Sala zitasaliwa katika sakafu na katika maeneo yasiyo na sakafu basi mikeka misafi kwa kila ibada itatumiwa. Aidha waumini wanaotaka kuleta mkeka au zulia binafsi kutoka nyumbani wataruhusiwa kufanya hivyo. Aidha mijimuiko baada ya Sala haitaruhusiwa.

Aidha kwa mujibu wa kanuni hizo Sala ya Itikafu haitasalia msikitini na pia waumini wametakiwa kula futari na daku nyumbani ni si Misikitini au katika Imambargah.

Wakati huo huo Pakistan imetangaza chanjo ya COVID-19 aina ya CanSino ambayo ni dozi moja itaanza kutolewa kote katika nchi hiyo kuanzia Aprili 5.

 

3474352/

captcha