Ijumaa ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ilitangazwa na mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Ruhullah Khomeini MA, kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Quds.
Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds nchini Iran yanafanyika kwa kushiriki wananchi katika maandamano baada ya kufanyika kwa miaka miwili kupitia misafara ya magari na kupitia intaneti kutokana na janga la corona.
Mbali na hapa nchini Iran, maandamano pia yamekuwa yakifanyika katika maeneo mbali mbali kote duniani na yataendelea wikiendi hii pia hasa katika nchi za Magharibi.
Wananchi wa Iran waliooshiriki katika maandamano ya leo wamesikika wakipiga nara za kuunga mkono taifa la Palestina linalodhulumiwa huku pia wakipiga nara za 'Mauti Kwa Israel', na 'Mauti kwa Marekani' sambamba na kulaani tawala za Kiarabu ambazo zimewasaliti Wapalestina kwa kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel.