IQNA

Waislamu Uswidi

Chama Kipya cha Waislamu Uswidi kushinikiza kuharamishwa kuvunjia heshima Qur'ani

21:20 - September 06, 2022
Habari ID: 3475744
TEHRAN (IQNA) - Chama kipya cha Waislamu nchini Uswidi (Sweden)kinataka kupiga marufuku kudhalilishwa kwa Qur'ani Tukufu.

Chama kipya cha Muslim Nuance Party kilichoanzishwa hivi karibuni kinashiriki katika uchaguzi ujao wa Uswidi unaopangwa kufanyika Septemba 11.

Kulingana na kiongozi wa chama Mikail Yüksel, uteketezaji moto Qur’ani Tukufu ni hatua "iliyolenga Waislamu moja kwa moja".

Nuance inajieleza kuwa ni chama kinachozingatia haki za walio wachache, huku Waislamu wakiwa ndio nguzo kuu. Wawakilishi wa Nuance wamesema kuwa vyama vilivyoanzishwa vimefeli kutetea jamii za wachache, na hasa Waislamu.

Pamoja na mambo mengine, chama hicho kinataka Sheria ya Sheria ya Kuwalinda Vijana (LVU) kutokana kwamba  mamlaka ya Uswidi inawateka nyara watoto wa Kiislamu.

"Tunataka kuchunguza taarifa za wazazi ambao wanahisi kuwa wametendewa isivyo haki", Mikail Yüksel aliambia shirika la utangazaji la taifa SVT.

Kwa ujumla, chama cha Nuance kilisema kilizingatia hasa matatizo matatu ambayo inaona kuwa ya dharura zaidi: Uislamu, ushirikiano na uhaba wa nyumba. Chama hicho kinalenga kuhakikisha kuwa Waislamu na Waswidi wenye asili ya Afrika wanapata hadhi maalum ya wachache katika katiba ya Uswidi.

Uchomaji wa Qur'ani umekuwa suala la dharura kufuatia hatua nyingi za mwanasiasa anayepinga uhamiaji mwenye uraia wa Denmark na Uswidi Rasmus Paludan. Mapema mwaka huu, maandamano wakati wa likizo ya Pasaka ya mwaka huu yalichochewa na hatua ya Paludan  kuteketeza moto Misahafu katika miji kadhaa ya Uswidi, ikiwa ni pamoja na Stockholm na Malmö. Maandamano hayo yalisababisha hasara kubwa nchini humo.

3480370

captcha