IQNA

Waislamu na Michezo

Wanamichezo Waislamu wenye ushawishi zaidi watajwa

22:05 - October 31, 2022
Habari ID: 3476013
TEHRAN (IQNA) – Mshambulizi maarufu Timu ya Taifa ya Soka ya Misri, Mohammed Salah, bingwa wa zamani wa uzito wa juu Mike Tyson, na mshindi wa taji la Ballon d'Or la mwanasoka bora duniani Karim Benzema ni miongoni mwa wanamichezo Waislamu wenye ushawishi mkubwa mwaka 2023.

Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya ‘The Muslim 500 2023’ iliyotolewa Jumapili ambayo inaorodhesha Waislamu wenye ushawishi mkubwa zaidi duniani. Pia ilimtaja mwanariadha wa Uingereza aliyefanikiwa zaidi katika historia, Farah Mohamed, mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa Zinedine Zidane, na Msenegali Sadio Mane wa Bayern Munich, kuwa kati ya wanamichezo Waislamu wenye ushawishi mkubwa zaidi wa 2023.

Wengine kwenye orodha hiyo ni pamoja na nyota wa zamani wa Manchester United, Paul Pogba ambaye mwaka 2019 alitangaza kusilimu na hivyo kuukumbatia Uislamu kama dini yake, na mmoja wa wanasoka mahiri barani Afrika kutoka Misri Mohamed Aboutrika. Aidha katika orodha hiyo yumo Wu lei, mchezaji mdogo zaidi wa kuwahi kucheza  ligi ya soka ya China akiwa na umri wa miaka 14 na kisha akawa mfungaji bora wa muda wote wa Shanghai SIPG akiwa na mabao 169.

3481075

captcha