IQNA

Shughuli za Qur'ani

Kituo cha Kiislamu cha Imam Ali (AS)

14:50 - November 09, 2022
Habari ID: 3476062
TEHRAN (IQNA) – Awamu ya Sita ya Mashindano ya Qur'ani Tukufu na Adhana kwa Waislamu wa Kaskazini mwa Ulaya itafanyika Februari.

Kituo cha Kiislamu cha Imam Ali (AS) huko Stockholm, Uswidi, kitakuwa mwenyeji wa mashindano hayo kuanzia Februari 24 hadi 26, 2023.

Mashindano hayo yatafanyika katika kategoria za usomaji wa Qur'ani, kuhifadhi Qur'ani, Adhana na Mafundisho ya Qur'ani.

Wasomaji au maqarii na wenye kuhifadhi Qur'ani pamoja na wenye kushindana Kuadhini  kutoka nchi tofauti za Ulaya wanatarajiwa kushiriki katika mashindano hayo.

Zoezi la kusajiliwa wanaotaka kushiriki mashindano hayo ya Qur'ani litsachapishwa kwenye tovuti ya kituo hicho na kurasa zake za mitandao ya kijamii hivi karibuni.

Hafla ya kufunga mashidano ya tano ya Qur'ani  mwaka huu ilifanyika katika kituo cha Eid Al-Ghadir ambapo washindani wakuu walitangazwa na kutunukiwa.

Kituo cha Kiislamu cha Imam Ali (AS) huandaa hafla mbalimbali za kidini na kitamaduni kwa mwaka mzima. Kituo cha Kiislamu cha Imam Ali (AS) ni taasisi huru ya kidini iliyooanzishwa na kundi la Waislamu wa Shia mwaka wa 1997. Kituo hiki kinadumisha shughuli za kawaida kama vile sala ya jumuiya ya kila siku, sala ya Ijumaa na sherehe nyingine za kidini na kitamaduni ambazo zinawavutia Waislamu eneo la Skandinavia.

4098202

captcha