IQNA

Kombe la Dunia Qatar

Amir wa Qatar afurahia ushindi wa Timu ya Taifa ya Soka ya Iran dhidi ya Wales

20:00 - November 25, 2022
Habari ID: 3476148
TEHRAN (IQNA)- Emir of Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani ameonekana akifurahia ushindi wa Timu ya Taifa ya Soka ya Iran wakati ilipoichapa Wales mabao 2 kwa 0 katika fainali za mashindano ya soka ya Kombe la Dunia yanayoendelea nchini Qatar.

Klipu iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii baada ya ushindi huo muhimu wa Timu ya Taifa ya Iran  katika mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Ahmad Bin Ali Stadium mjini Rayyán leo Ijumaa, Emir wa Qatar alionekana akifurahia ushindi huo akiwa katika jukwaa la wageni maalumu.

Vijana wa Kocha Mreno Carlos Queiroz leo waliingia dimbani katika mechi ya kundi B wakiwa na jeraha kubwa la kufungwa mabao 6 kwa mawili na Uingereza katika mechi yao ya awali. Timu ya soka ya Iran ambayo pia ni maarufu "Team Melli" ilionekana kuwa na shauku kubwa ya kupata ushindi na ilianza kusakata kandanda safi tangu dakika ya mwanzo baada ya kipyenga cha kuanza mechi kupulizwa.

Iran ambayo katika mechi ya awali licha ya kupoteza mchezo huo ilimpoteza pia kipa wake mahiri nambari moja Alireza Beiranvand ambaye aliumia vibaya puani, lango lake leo lilindwa vyema na golikipa wake nambari mbili Sayyid Hussein Hussein.

Iran beats 10-man Wales to keep World Cup qualification hopes alive | CNN

Kipindi cha kwanza kilimalizika huku Iran ikitawala mchezo lakini ikishindwa kutikisa nyavu za Wales. Washambuliaji mahiri wa Iran kama Sardar Azmon anayesakata soka la kulipwa katika ligi ya Bundesliga ya Ujerumani na Ali Gholizadeh anayesakata kambumbu la kimataifa huko nchini Ubegiji walikosa nafasi kadhaa za kufunga baada ya mashuti yao kugonga mwamba.

Mambo yalianza kuindea vizuri zaidi Iran baada ya mlinda mlango wa Wales kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika dakika ya 86 baada ya kumchezea rafu nyota hatari wa Iran Mehdi Taremi mchezaji mahiri wa Porto ya Ureno.

Magoli ya Iran katika mechi ya leo yaliyohuisha matumaini ya Iran kusonga mbele katika kundi lake kama itashinda katika mechi iliyobakia na Marekani yalipachikwa wavuni muda wa ziada na kiungo Ruzbeh Cheshmi katika dakika ya 98 na beki wa kulia Ramin Rezaeian dakika ya 101. Mabao yote ya Iran yalifungwa katika dakika za nyongeza za mchezo huku mabeki wa Iran wakifanikiwa kuwatia mfukoni nyota wa timu ya soka ya Wales akiwemo nahodha na mchezaji wao mahiri Gareth Bale. Miji mbalimbali ya Iran leo imeshuhudia furaha, nderemo na vifijo vya kushangilia ushindi wa timu ya soka ya Iran katika mashindano ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

4102265

captcha