IQNA

Shughuli za Qur'ani

Rais wa Mauritania atembelea maonesho ya Qur'ani Tukufu mjini Nouakchott

21:17 - January 07, 2023
Habari ID: 3476370
TEHRAN (IQNA) – Rais wa Mauritania Mohamed Ould Ghazouani ametembelea maonyesho ya Qur'ani Tukufu katika mji mkuu wa nchi hiyo Nouakchott.

Maonyesho hayo yametajwa kuwa  sehemu ya mfululizo wa maonyesho yanayofanyika mjini Nouakchott ndani ya mfumo wa shughuli za kuadhimisha Nouakchott kama Mji Mkuu wa Utamaduni wa Ulimwengu wa Kiislamu mnamo 2023.

Ghazouani alitembelea maonyesho hayo ambayo yana nakala za Qur'ani, shughuli za Qur'ani, mbinu zinazotumiwa nchini humo kufundisha Qur'ani na mfano wa mji wa kihistoria wa Qana.

Pia aliona Msahafu unaojulikana kama Muati Maulana Mus’haf ambao umeandikwa kwa mkono kwa njia ya kaligrafia  nchini Mauritania na ndiyo nakala kubwa zaidi ya Quran iliyoandikwa kwa mbinu ya Warsh.

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (ISESCO) limechagua Nouakchott kama mji mkuu wa kitamaduni wa Ulimwengu wa Kiislamu mnamo 2023.

Vipindi vya kuadhimisha tukio hilo vimeratibiwa kushirikishwa na idadi ya mawaziri na maafisa wa kitamaduni wa nchi za Kiislamu na Kiarabu.

Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania ni nchi iliyoko katika eneo la Maghreb magharibi mwa Afrika Kaskazini.

Idadi ya watu nchini humo inakadiriwa kuwa takriban milioni 4 na takriban Wamauritania wote ni Waislamu.

Shughuli na programu za Qur'ani ni maarufu sana katika nchi ya Kiafrika.

4112693

captcha