IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Waislamu wasambaza waridi katika Makanisa ya Uturuki kujibu kuvunjiwa heshima Qur'ani nchini Uswidi

17:43 - January 23, 2023
Habari ID: 3476449
TEHRAN (IQNA) – Kufuatia kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Uswidi (Sweden) kikundi cha vijana kusini mashariki mwa Uturuki kilisambaza maua ya waridi makanisani.

Vijana katika wilaya ya kati ya Artuklu mkoa wa Mardin walizuru makanisa siku ya Jumapili wakiwa na maua ya waridi mkononi, na kuwakabidhi viongozi wa kanisa hilo na kulaani kuteketezwa moto nakala ya Qur'ani Tukufu  nje ya Ubalozi wa Uturuki mjini Stockholm siku ya Jumamosi.

Mmoja wa vijana katika kundi hilo alikuwa Ibrahim Halil Yetim, ambaye alirekodi jitihada zao kwenye video.

Alisema kuwa, wakiwa vijana wa Kiislamu, walifikiria jinsi ya kukabiliana tukio ovu la Uswidi na kuamua kufuata ushauri wa Mtume Muhammad (SAW) kwa kuzuru makanisa na kueleza hisia zao kwa njia inayolingana na dini yao.

Rasmus Paludan, kinara wa chama cha misimamo mikali ya mrengo wa kulia cha Denmark kijulikanaco kama Stram Kurs (Msimamo Mkali), alipewa ruhusa na serikali ya Uswidi kuchoma Qur'ani Tukufu nje ya Ubalozi wa Uturuki huko Stockholm.

Kwa kujibu hatua ya Uswidi ya kuidhinisha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu, Ankara imebatilisha ziara tarajiwa ya  Waziri wa Ulinzi wa Uswidi Pal Jonson huko Uturuki.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki siku ya Ijumaa ilimwita Balozi wa Uswidi mjini Ankara Staffan Herrstrom, ambaye aliambiwa kwamba Uturuki "inalaani vikali kitendo hiki cha uchochezi, ambacho ni uhalifu wa chuki, kwamba mtazamo wa Uswidi haukubaliki, kwamba Ankara inatarajia kitendo hicho hakiruhusiwi, na matusi kwa maadili matakatifu hayawezi kutetewa chini ya kivuli cha haki za kidemokrasia".

Wananchi wa mataifa mbalimbali ya Kiislamu na yasiyo ya Kiislamu wameendelea kulaani hatua ya kuchomwa moto nakala ya Qur'ani Tukufu nchini Sweden.

Maandamano ya kulaani kitendo hicho yameendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya dunia sambamba na kutaka kuchukuliwa hatua kali za kuzuia kukaririwa kitendo kama hicho huku tawala na serikali mbalimbali zikitoa taarifa ya kulaani kitendo hicho..

Iran, Jordan, Kuwait, Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu, na Pakistani ni miongoni mwa nchi ambazo zimetoa taarifa kali kulaani kudhalilishwa kwa maandishi matakatifu ya Kiislamu.

Aidha, Katibu Mkuu wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi (P-GCC) Nayef Falah al-Hajraf alikemea mamlaka ya Uswidi kwa kuruhusu mtu mwenye itikadi kali kuchoma Qur'ani Tukufu mbele ya ubalozi wa Uturuki mjini Stockholm, na kusema kitendo hicho kitachochea hisia za Waislamu duniani kote."

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) Hussein Ibrahim Taha Katibu naye pia amelaani jinai iliyofanywa na baadhi ya wanachama wa mrengo wa kulia wenye misimamo mikali ya kuchoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu huko Stockholm Sweden.

3482183

captcha