IQNA

Harakati za Qur'ani

Zaidi ya wanafunzi 250 waliohifadhi Qur'ani Tukufu waenziwa Tokat, Uturuki

16:19 - January 28, 2023
Habari ID: 3476478
TEHRAN (IQNA) - Sherehe ilifanyika katika Mkoa wa Tokat, kaskazini mwa Uturuki, kwa ajili ya kuwapongeza wanafunzi 258 ambao wameweza kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na idadi kubwa ya watu na viongozi akiwemo Mkuu wa Masuala ya Kidini nchini Turuku Ali Erbas katika Msikiti wa Gazi Osman Paşa katika eneo hilo.

Vyeti vya kuhifadhi na zawadi zilitolewa kwa wavulana 120 na wasichana 138 wa kukariri.

Akihutubia katika hafla hiyo, Erbas alisema misikiti nchini Uturuki inatoa kozi za usomaji na kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa raia wote.

"Qur'ani Tukufu ndio muujiza mkubwa na Mwenyezi Mungu ndiye aliyeiteremsha ili iwaongoze watu kutoka gizani kwenda kwenye nuru," alisema.

Kwa mujibu wa maafisa wa Uturuki, takriban 12,500 waliweza kuhifadhi Qur'ani Tukufu nchini humo mwaka jana.

Qur'ani Tukufu ndiyo maandiko pekee ya kidini ambayo yanahifadhiwa kikamilifu na wafuasi wake.

Watu wasiohesabika katika kila umma wa Kiislamu wamehifadhi Quran tangu siku ya kwanza ilipoteremshwa.

Quran ina Juzuu (sehemu) 30, sura 114, na aya 6,236.

4117687

captcha