IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Kituo cha Dar-ul-Quran Imam Ali (+Picha)

23:42 - February 12, 2023
Habari ID: 3476552
TEHRAN (IQNA) - Washindi wakuu walitangazwa na kutunukiwa tuzo katika hafla ya kufunga Mashindano ya 16 ya Qur'ani Tukufu ya Kituo cha Dar-ul-Quran cha Imam Ali (AS) nchini Iran.

Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Sheikh Saduq katika Haram ya Hazrat Abdul Azim Hassani (AS) eneo la  Rey, Kusini mwa Tehran, sanjari na sherehe za kuadhimisha mwaka wa 44 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979.

Baada ya  wimbo wa taifa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na kusomwa aya za Qur'ani na Ustadh Yunes Shahmoradi, Mkurugenzi wa Kituo cha Dar-ul-Quran cha  Imam Ali (AS)Mohammad Ansari alipanda jukwaa, akisisitiza hadhi adhimu ya Qur’ani Tukufu.

Alisema Qur’ani Tukufu ni mwongozo kwa wanadamu wote na kwamba kupata wokovu kunahitaji kufanyia kazi mafundisho ya kitabu hiki cha Mwenyezi Mungu.

Alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kupata nafasi ya kuandaa mashindano hayo ya 16, ambapo alisema jumla ya wanaume na wanawake 14,230 kutoka maeneo mbali mbali ya Iran pamoja na nchi nyingine walichuana katika mchujo ambapo kulikuwa na makundi mawili ya umri wa miaka 18 na chini na zaidi ya 18.

Kategoria hizo zilijumuisha usomaji wa Qur’ani Tukufu, Tarteel, Kuhifadhi na ufahamu wa maana ya aya za Qur’ani Tukufu.

Alisema zaidi ya washiriki 570 wanatoka nchi kama vile Afghanistan, Iraq, Bahrain, Tajikistan, Nigeria, Bangladesh, Syria, Kenya na Ivory Coast.

Amebainisha kuwa wataalamu 82 wa Qur'ani katika kitengo cha wanaume na wataalamu 59 wa Qur'ani katika sehemu ya wanawake walihudumu katika jopo la majaji.

Ansari aliendelea kusema kuwa moja ya malengo ya mashindano hayo ya kila ni kukuza mafundisho ya Qur'ani Tukufu miongoni mwa watu katika jamii, na kubainisha kuwa Mtume Mtukufu Muhammad (SAW) amesema: "Waliobora katika nyinyi ni wale wanaojifunza Qur'ani na kuifundisha kwa wengine”.

Abbas Salimi, afisa wa  Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu  Hazrat Abdul Azim Hassani (AS), na alikuwa miongoni mwa wazungumzaji wengine katika hafla hiyo.

Mwishoni mwa hafla hiyo, washindi wa kategoria tofauti katika sehemu na rika tofauti walitajwa na kupokea tuzo zao.

 

3482434

captcha