IQNA

Waislamu India

Wanafunzi wa Kiislamu wanataka Mahakama ya India iruhusu Hijabu kwenye mitihani

12:22 - February 23, 2023
Habari ID: 3476614
TEHRAN (IQNA) – Wanafunzi Waislamu wa kike nchini India Jumatano wamewasilisha ombi katika Mahakama ya Juu ya India wakitaka waruhusiwe kufanya mitihani ya kila mwaka ya vyuo vya Karnataka wakiwa wamevalia vazi la staha la Hijabu.

Akiwakilisha kundi la wanafunzi kutoka Karnataka, wakili Shadan Farasat alihimiza jopo la majaji linalojumuisha Jaji Mkuu DY Chandrachud na Jaji PS Narasimha kuorodhesha ombi la dharura la kutaka mahakama kuu iidhinishe haki ya wanafunzi wa kike wa Kiislamu kuvaa Hijabu wakati wa mitihani ya kila mwaka. vyuo vya Karnataka. Mitihani ya kila mwaka imepangwa kuanza Machi 9, 2023.

Mwaka jana Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetangaza kuwa mamlaka nchini India zinazidi kuwakandamiza na kuwaadhibu Waislamu nchini humo.

Marufuku kwa hijabu katika vyuo na baadhi ya shule katika jimbo la kusini mwa India la Karnataka mwaka jana ni jambo ambalo limezua mzozo huku kukiwa na wasiwasi unaoongezeka kwamba mashambulizi dhidi ya nembo na desturi za Waislamu ni sehemu ya ajenda kubwa ya Wahindu ya mrengo wa kulia ya kuwalazimisha walio wachache kufuata itikadi za waliowengi.

Waislamu milioni 200 walio wachache nchini India wanasema kupigwa marufuku kwa hijab kunakiuka uhuru wao wa kidini, unaohakikishwa chini ya katiba ya India.

3482577

Kishikizo: hijabu india karnataka
captcha