IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Kuhifadhi Qur’ani ya Qatar kurushwa hewani Mwezi wa Ramadhani

13:48 - March 23, 2023
Habari ID: 3476747
TEHRAN (IQNA) – Vipindi vya toleo la sita la Tuzo ya Katara ya Kuhifadhi Qur’ani Tukufu vitaonyeshwa kwenye Televisheni ya Qatar katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Taasisi ya Katara ya  Kijiji cha Utamaduni imetangaza kuzindua vipindi vya Tuzo ya Katara ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu kupitia Qatar TV katika kipindi chote cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Washiriki 100 waliofika fainali waliochaguliwa na kamati ya uchunguzi kati ya washiriki 1,273, ambapo huwakilisha  nchi 13 za Kiarabu na nchi 18 zisizo za Kiarabu. Washiriki 58 kutoka nchi za Kiarabu walihitimu.

Washiriki wa fainali ya Tuzo ya Katara ya Kuhifadhi Qur'ani katika hatua zake tatu walieleza furaha yao ya kufuzu kwa hatua ya awali ya mchujo, inayojumuisha washiriki 100. Wametaja tuzo hiyo kuwa ni miongoni mwa mashindano yenye nguvu ya kimataifa kutokana na kujumuisha washiriki wengi kutoka mataifa mbalimbali duniani.

3482920

Kishikizo: qurani tukufu katara
captcha