IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Dua za Kila Siku za Mwezi wa Ramadhani- Siku ya Nane

11:24 - March 30, 2023
Habari ID: 3476782
Dua hizi za kila siku za Mwezi wa Ramadhani husomwa toka mwanzo ya tarehe mosi Ramadhani hadi siku ya mwisho katika mwezi huu mtukufu. Kila dua ina siku yake, na inaweza kusomwa mara nyingi kadiri ya uwezo wa mtu mwenyewe.

Ramadan Daily Supplications: Day 8

Ee Mwenyezi Mungu! Niruzuku katika mwezi huu (ili niweze) kuwasaidia mayatima, niwalishe vyakula, pia nijaalie niweze kuwasalimia (Waislamu wote) kila nikutanapo nao, Unijaalie kuhusubiana na watukufu (uwapendao) kwa utajiri wako Ewe Makimbilio wa wahitaji.

Habari zinazohusiana
captcha