IQNA

Mapambano ya Kiislamu (Al-Muqawama Al-Islamiya)

Viongozi wa Hizbullah, Hamas na Jihad Islami wasisitiza kutoa jibu la pamoja dhidi ya Israel

14:12 - September 03, 2023
Habari ID: 3477543
TEHRAN (IQNA)- Viongozi wa harakati za mapambano ya Kiislamu (Al-Muqawama Al-Islamiya) za Palestina na Lebanon wameapa kushirikiana ili kutoa jibu la pamoja dhidi ya sera za uvamizi za utawala haramu wa Israel.

Hapo jana, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrallah aliwapokea mjini Beirut, Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS, Saleh al-Arouri, na Ziad al-Nakhalah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami. 

Viongozi hao wamesema wana azma thabiti ya kuileta pamoja kambi ya muqawama ili itoe pigo kwa utawala wa Kizayuni na sera zake za kibeberu na uporaji wa ardhi.

Wamesisitiza kuwa kuna haja ya kudumisha ushirikiano na mawasiliano baina ya harakati za muqawama hasa za Palestina na Lebanon, na kufuatilia kwa jicho la karibu matukio yote ya kisiasa, kiusalama na kijeshi katika eneo ili maamuzi mwafaka yatolewe.

Kadhalika wakuu hao wa mrengo wa muqawama katika eneo la Asia Magharibi wamechunguza hali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unalokaliwa kwa mabavu, na kuimarika harakati za muqawama katika eneo hilo.

Aidha katika mkutano huo wa jana Jumamosi mjini Beiruit, vinara hao wa muqawama katika nchi za Lebanon na Palestina wamejadili vitisho vilivyotolewa hivi karibuni na utawala wa Kizayuni wa Israel na njia za kuvikabili.

3485014

Habari zinazohusiana
captcha