IQNA

Jinai za Israel

Idadi halisi ya askari wa Israeli walioangamizwa katika Kimbunga cha Al-Aqsa yazidi kufichuka

18:19 - November 28, 2023
Habari ID: 3477959
Jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel limekiri kuwa zaidi ya askari wake 1,000 wa walowezi wa utawala huo waliuawa wakati wa mapigano ya Kimbunga cha Al-Aqsa.

 Kulingana na duru za Kizayuni, idadi ya Wazayuni waliouawa katika mapigano ya Kimbunga cha Al-Aqsa ni takriban 1,500, ambapo zaidi ya 380 ni wanajeshi.

Imeelezwa katika ripoti hiyo kuwa duru za muqawama zimesema, idadi ya wanajeshi wa Kizayuni waliouawa katika vita vya Gaza kuwa kubwa zaidi kuliko takwimu zilizotangazwa na Wazayuni hao na kuongeza kuwa, wanajeshi 50 wa Kizayuni walizikwa ndani ya siku moja tu.

Kuhani mmoja wa Kizayuni amefichua kuhusu hasara ulizopata utawala wa Kizayuni wakati wa shambulio la ardhini ulilofanya katika Ukanda wa Gaza, akimnukuu askari mmoja wa utawala huo, na kutangaza kuwa katika usiku mmoja tu, vifaru vitatu vya kivita vya aina ya "Tiger" viliteketezwa na wanajeshi 36 wa Kizayuni pia waliangamizwa.

Vita vya pamoja vilivyoongozwa na Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS dhidi ya utawala wa Kizayuni, vilivyoanza Oktoba 7 kwa anuani ya Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa na kusimamishwa kwa muda Ijumaa iliyopita  ya tarehe 24 Novemba vilikuwa ni vita nadra kushuhudiwa ambapo mirengo mitatu ya Muqawama katika eneo ya Hizbullah ya Lebanon, Ansarullah ya Yemen pamoja na makundi ya Muqawama ya Iraq ilipigana bega kwa bega na Muqawama wa Palestina ambapo mirengo yote hiyo minne ya Muqawama wa Kiislamu katika eneo yalijipanga pamoja dhidi ya utawala dhalimu wa Kizayuni.

Wakati huo huo Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Qatar na Harakati ya Hamas zimetangaza kuwa, makubaliano ya usitishaji vita huko Gaza yameongezwa muda kwa siku mbili zaidi, kwa msingi wa masharti yale yale ya awali.

Baada ya kumalizika usitishaji vita wa siku nne ulioanza Ijumaa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imetangaza kuwa usitishaji mapigano  huko Gaza umeongezwa muda wa siku mbili zaidi.

Huku ikithibitisha makubaliano hayo, harakati ya Hamas imesema: Tumekubaliana na ndugu zetu wa Misri na Qatar juu ya kurefushwa kwa muda usitishaji vita kwa siku nyingine mbili kwa masharti yale yale ya awali.

4184641

Habari zinazohusiana
captcha