IQNA

Israel inawashikilia watoto 93 wa Palestina katika jela ya Ofer

21:45 - June 08, 2015
Habari ID: 3312263
Watoto 93 Wapalestina hivi sasa wanashikiliwa katika Jela ya kuogofya ya Ofer ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya Masuala ya Wafungwa Katika Mamlaka ya Ndani ya Palestina, watoto 28 kati ya wanaoshikiliwa katika gereza hilo lililoko karibu na mji wa Ramallah Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, wanaugua magonjwa mbalimbali. Ripoti hiyo pia imesema watoto 161 Wapalestina walio chini ya umri wa miaka 18 walikamatwa na wanajeshi wa Israel katika kipindi cha mwanzoni wa mwaka huu wa 2015 hadi mwisho wa mwezi Mei.

Wanajeshi wa utawala dhalimu wa Israel wanakanyaga haki za kimsingi za watoto hao. Kwa ujumla watoto takriban 200 wanashikiliwa katika korokoro za Israel wakiwemo watoto 26 walio chini ya umri wa miaka 16. Mwaka jana Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Watoto DCI lilisema, wakuu wa Israel wamekataa kuwapa asilimia 93 ya watoto hao haki ya kuwa na wakili. Mkuu wa Idara ya Wafungwa Katika Mamlaka ya Ndani ya Palestina Issa Qaraqe amesema makachero wa Israel wanatumia ukatili na unyama kuwalazimisha watoto Wapalestina wakiri makosa ambayo hawajatenda. Kwa ujumla kuna Wapalestina wapatao 7,000 wanaoshikiliwa mateka katika jela za kutisha za utawala haramu wa Israel. Kiujumla ni kuwa, katika kipindi cha miaka 48 iliyopita Wapalestina laki nane na nusu wametiwa nguvuni na utawala wa Kizayuni wa Israel.../mh

3312080

captcha