IQNA

Watetezi wa Palestina

Wananchi wa Iran waandamana kulaani utawala wa Israel unaoua watoto

21:46 - November 19, 2023
Habari ID: 3477915
TEHRAN (IQNA)- Watu wa Iran ya Kiislamu jana Jumamosi walishiriki katika maandamano makubwa kote nchini kuwatetea watoto wanaoendelea kuuawa wa Palestina sambamba na kulaani "mauaji ya watoto wachanga", "uhalifu", "mauaji ya kimbari", "mauaji ya halaiki", "ugaidi", "uhalifu wa kivita" na "maafa ya binadamu" yanayoendelea katika Ukanda wa Gaza.

Wananchi wa Iran ya Kiislamu kote nchini wamefanya maandamano wakieleza masikitiko na mshikamano wao na kina mama wa mashahidi wa Gaza, na kutangaza chuki na hasira zao kutokana na uovu unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel. Waandamanaji hao wamezitaka jumuiya za kimataifa kusitisha mauaji ya utawala haramu wa Israel na kuwahudumia watu waliopatwa na maafa wa Palestina huko katika Ukanda wa Gaza.

Katika maandamano hayo wananchi wa miji na vijiji vya Iran wamelaani jinai za utawala katili wa Israel dhidi ya watoto wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza na kusisitiza udharura wa kusitishwa mara moja jinai za utawala huo ghasibu.

Wananchi wa Iran pia wametoa nara dhidi ya utawala wa Israel, na kulaani vikali mashambulizi yanayolenga hospitali na mauaji ya kikatili ya watoto wa Kipalestina.

Maandamano kama haya ya kulaani uhalifu unaofanywa na Israel kwa msaada na himaya ya baadhi ya nchi za Magharibi huko Gaza yanaendelea kufanyika katika pembe mbalimbali duniani. 

/4182512

Habari zinazohusiana
captcha