IQNA

Jinai za Israel

Msikiti mkongwe wa Gaza walengwa katika shambulio la anga la Israel

17:05 - November 18, 2023
Habari ID: 3477910
AL-QUDS (IQNA) - Msikiti wa Jamia wa Omari, ambao ni moja ya misikiti mikongwe zaidi katika Jiji la Kale la Gaza, uliripotiwa kulengwa katika mashambulizi ya anga ya utawala katili wa Israel siku ya Alhamisi.

Televisheni ya Al Jazeera imechapisha ripoti ya hujuma hiyo bila kutoa maelezo zaidi kuhusu ukubwa wa uharibifu huo.

Msikiti huo, unaojulikana pia kama Msikiti Mkuu wa Gaza, ulijengwa katika kipindi cha Bani Umayya karibu mwaka 700 Miladia.

Mnara wa msikiti, na msingi wake wa mraba na mnara wa pembetatu, ulijengwa wakati wa utawala wa Milki ya Mamluk huko Gaza kutoka 1250 hadi 1517 Miladia.

Tokea mwaka 2006,  mashambulizi ya Israel huko Gaza yamekuwa yakilenga kwa makusudi  turathi za eneo hilo ambazo kimsingi huwapa wakazi wake utambulisho.

Mnamo mwaka wa 2014, msikiti mwingine unaoitwa Omari, ulioko katika eneo la Jabaliya karibu na Gaza City, ulipigwa na kombora la Israel, na kusababisha kifo cha muezzin pamoja na uharibifu mkubwa.

Mji Mkongwe wa Gaza una maeneo kadhaa ya  kihistoria ikiwa niapamoja na Kanisa la St Philip the Evangelist Chapel na Kanisa la St Porphyrius.

Kanisa la St Porphyrius lililojengwa miaka 1,600  lililipuliwa na jeshi katili la Israel mwezi Oktoba, wakati Waislamu na Wakristo walikuwa wamekimbilia eneo hilo kupata hifadhi wakati wa vita.

Kanisa hilo, lililojengwa awali mwaka wa 425 Miladia na lilipewa jina la Mtakatifu Porphyrius, ni mahali pa kale zaidi pa ibada ya Kikristo huko Gaza.

Shambulio hilo la Israel liliharibu kumbi mbili zilizopakana na jengo la kanisa hilo na kusababisha vifo vya takriban watu 18 waliokuwa wakitafuta hifadhi kwenye uwanja wa kanisa hilo.

Kanisa hilo liligeuzwa kuwa msikiti wakati wa utawala wa Wamamluk wa karne ya saba, lakini lilirudishwa kwenye wakfu wake wa awali wa Kikristo katikati ya karne ya 12.

captcha