IQNA

Bintiye Imam Khomeini (MA) kuhutubu katika Siku ya Quds Afrika Kusini

19:35 - May 12, 2020
Habari ID: 3472758
TEHRAN (IQNA) – Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds ya mwaka huu yanatazamiwa kufanyika katika ukumbi wa Instagram na mitandao mingine ya kijamii nchini Afrika Kusini, kutokana na janga la corona.

Shakhsia mbali mbali wa kimataifa wanatazamiwa kutoa hotuba zao kwa njia ya intaneti na mitandao hiyo ya kijamii siku hiyo ambayo huadhimishwa Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Baadhi ya shakhsia hao ni Dakta Zahra Mostafavi, binti ya hayati Imam Khomeini MA Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Dkt Hossein Amir-Abdollahian, Msaidizi Maalumu wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya kimataifa, na Ndaba Mandela, mjukuu wa Nelson Mandela, mwanamapambano wa ubaguzi na Rais wa kwanza Mwafrika wa Afrika Kusini.

Wengine ni Geoff Makhubo, Meya wa jiji la Johannesburg, Khaled al-Qodoumi, mwakilishi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS nchini Iran, Nasser Abousharif, mwakilishi wa harakati ya Jihadul Islami ya Palestina mjini Tehran, Gavana Mkuu wa mkoa wa Cape Town, Ebrahim Rasool na Masoud Shajareh, afisa wa Kamisheni ya Kiislamu ya Haki za Binadamu ya Uingereza, pamoja na shakhsia wengine wa kimataifa.

Imam Khomeini MA Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alitangaza kuwa Ijumaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni Siku ya Kimataifa ya Quds. 

Waislamu na wapenda haki wamekuwa wakifanya maandamano katika pembe mbalimbali za dunia kila mwaka katika Siku ya Kimataifa ya Quds, na kubainisha hasira zao kwa siasa za kibaguzi na kikatili zinazotekelezwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.

3898399/

captcha