IQNA

Diplomasia

Afrika Kusini yamuondoa balozi wake Israel kulalamikia kuendelea jinai dhidi ya Wapalestina Gaza

21:31 - November 07, 2023
Habari ID: 3477856
PRETORIA (IQNA)- Vyombo vya habari vya Magharibi viliripoti jana Jumatatu kuwa, Afrika Kusini imewarudisha nyuma wanadiplomasia wake kutoka ardhi zinazokaliwa kwa mabavu kulalamikia kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni huko Ghaza.

Wanadiplomasia wa Afrika Kusini wameitwa kurejea nchini kwao kwa ajili ya mashauriano zaidi kuhusiana na jinai hizo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Naledi Pandor alisema hayo Jumatatu na kuongeza kuwa wanadiplomasia hao wameitwa nyumbani ili kubaini iwapo wanaweza kusaidia kujua ikiwa uhusianao wa kidiplomasia wa nchi mbili unaweza kuendelezwa katika hali zote au la.

Alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari baadaye kwamba taifa hilo la Afrika "linasikitishwa sana na kuendelea mauaji ya watoto na raia wasio na hatia katika maeneo ya Palestina." "Tuliona ni muhimu kwamba tuonyeshe wasiwasi wa Afrika Kusini huku tukiendelea kutoa wito wa kusitishwa kwa kina [kwa uhasama]."

Chad nayo pia imemwita nyumbani Balozi wake Mdogo huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel) kufuatia kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya raia wa Kipalestina wa Ukanda wa Gaza huku wimbi la maandamano na malalamiko yakiendelea kushuhudiwa katika nchi mbalimbali dunia kulaani jinai za utawala wa Kizayuni.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Chad imetoa taarifa na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni huko Ukanda wa Gaza na kutangaza kuwa imemrejesha nyumbani Balozi Mdogo wa nchi hiyo huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu kwa ajili ya mashauriano na majadiliano kutokana na hali ya mgogoro wa kibinadamu inayoshuhudiwa sasa huko Ukanda wa Gaza.  

Wizara ya Mambo ya Nje ya Chad pia imesisitiza kuwa kuna ulazima wa kusitishwa jinai za utawala wa Kizayuni huko Gaza na kutekelezwa usitishaji vita katika eneo hilo.  Huku jinai za utawala ghasibu wa Kizayuni dhidi ya wakazi wa Kipalestina  wa Ukanda wa Gaza zikiendelea kila uchao, idadi ya serikali zinazopinga jinai hizo pia inaongezeka siku baada ya siku. 

3485905

Habari zinazohusiana
captcha